Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 30, 2012

CCM INAPASWA KUCHUKUA HATUA NZEGA


Hivi hali hii ni mpaka lini?....au ndio kusema Chama kinashindwa kuonesha uwezo wake katika kuchukua maamuzi kwa wanachama wake wanapofikia hatua za kurumbana kwa muda mrefu kiasi hiki.

Tunawezaje kuendelea kukiamini Chama hiki ikiwa makundi yanaendelea kuleta athari kubwa kiasi ambacho sasa zinaelekea hata kutishiana uhai....au tuseme Chama kinabariki marumbano haya au kuna baadhi ya viongozi wanamaslahi na mivutano ya wanachama isiyokwisha....?

Wakazi wa Nzega wamekuwa ni mashahidi wa marumbano baina ya wanachama wawili wa CCM wilayani humo,Hussein Bashe na Hamisi Kigwangala,ambayo yanaripotiwa chokochoko zake zilianzia wakati wa kura za maoni kuwania nafasi ya kuteuliwa na Chama chao kuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega.

Hata hivyo ilikuwa ni sehemu ya kuonesha kuwa marumbano hayo yamefikia mwisho pindi Chama kilipomteua Hamisi Kigwangala kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM licha ya kuwa alikuwa amezidiwa kwa kura nyingi na Hussein Bashe ambaye aliibuka mshindi wa kwanza katika kura hizo za maoni ambazo kwa sehemu kubwa zilizua mgogoro wa muda mrefu.

Hakuna haja ya kuzama ndani zaidi juu ya yale yaliyojitokeza huko Nzega,lakini kwasasa kuna haja kwa CCM kuanzia ngazi ya Taifa kuliona hilo kwani limefikia hatua ya kutaka kuonesha wazi kuwa Chama kinaelekea kubaya sana na hasa inapofikia hatua ya wanachama tena viongozi  kushikiana bastola hadharani na tena kibaya zaidi nyakati hizi za uchaguzi ndani ya Chama......AIBU AU FEDHEHA?

CCM inapaswa kutambua wananchi wa sasa sio wale wa zamani,ikumbukwe CCM ndio imekuwa ikitamba kwamba  inalinda na kutetea amani ya nchi hii,sasa leo imekuwaje viongozi wake kuanza kutishiana maisha kwa mtutu wa bunduki?.......


 

No comments: