Pages

KAPIPI TV

Saturday, July 28, 2012

OPARESHENI AMKA NZEGA INAELEKEA KUZAA MATUNDA!


Hamisi Kigwangalla
6:14am Jul 28
Amka Nzega! Amka Nzega! Amka Nzega! Operation 'amka nzega' tuliyoianzisha jimboni kwetu mara tu baada ya mimi kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la nzega inaelekea kuzaa matunda,
Sasa tutapata ushuru wa huduma (service levy) wa asilimia 0.3 ya turnover net of VAT and excise duty kwa miaka yote 14 ya uwepo wa Golden Pride Project Nzega, na watalipa with surcharge ya 1% ya malimbikizo yote, tumewabana hawana pa kutokea, watalipa tu! 
Pia watalipa kifuta jasho kwa wachimbaji wadogo wadogo, watafanya matengenezo ya mradi wa maji safi Nzega, watajenga barabara za lami na high school na health centers Nzega, watakamilisha ahadi zao zote za miradi ya maendeleo kabla hawajaondoka Nzega - 
Na wasipoturidhisha sisi yafuatayo yatatokea, watanyimwa leseni ya kusafirisha dhahabu nje, halmashauri itashikilia mali za mgodi kwa nguvu ya sheria zetu, watanyimwa kibali cha kuanzisha mgodi mwingine Nyakafuru (ambapo wanapanga kuhamishia mashine za Nzega baada ya kufunga mgodi), watanyimwa leseni za utafiti wa madini, watachafuka kimataifa! 
Haya yote wanatakiwa kuyafanya la sivyo watapata adhabu hizo tulizozisema...yote haya yakishindikana tutaandamana kuelekea mgodini kama tulivyoazimia siku ya tarehe 16 Juni 2012! "Nzega yetu, ama mwisho wetu - tutashinda!"

No comments: