Pages

KAPIPI TV

Sunday, July 29, 2012

BUNDA YAKAMILISHA ZOEZI LA USAILI WA MAKARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012.

.
Na Berensi Alikadi-Bunda.
 
WILAYA ya Bunda mkoani  imekamilisha  zoezi la usaili wa makarani wa sensa watakaohusika katika kazi ya kuhesabu watu katika wilaya hiyo Agost 26 mwaka huu.
 
Mwenyekiti wa kamati ya sensa  ya wilaya hiyo Joshua Mirumbe amesema jana kuwa zoezi hilo limeenda vizuri katika vijiji vyote vya tarafa nne za wilaya hiyo ambazo ni Nansimo,Kenkyombyo,Chamliho na Serengeti.
 
Joshua ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa kilichobaki sasa ni kuyachambua majina hayo na kuona wale waliokidhi vigezo ambao alisema kuwa ndio watakaochukuliwa kwa ajili  ya kufanya kazi ya sensa na wala si vinginevyo.
 
‘’Pamoja na kufanya usaili huo kilichobaki sasa ni kuchanbua majina ya wale waliokidhi vigezo tu ndio watakaochukuliwa maana hili zoezi ni la kitaifa hatuwezi kuchukuwa kila mtu hata wale wasiokuwa na sifa maana likiharibika ni aibu kwa wilaya yetu.’’alisema Mirumbe.
 
Alifafanua kuwa baada ya kamati ya wilaya kupitia majina hayo na kuchagua yanayofaa yatapelekwa katika vijiji husika kwa ili waliochaguliwa waweze kujiandaa kwa ajili ya semina ambayo alisema itaanza muda si mrefu. Katika tarafa zote nne za wilaya hiyo.
 
Aidha mwenyekiti huyo alirudia wito wake wa kuwataka viongozi wa dini. Vyama ,mashirika yasiyokuwa ya kiserikali,maafisa tarafa watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wanahamasisha wananchi ili waweze kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo .
 
Alitoa onyo kwa mtu yeyote au kikundi cha watu ama dhehebu la dini litakalogomesha zoezi hilo litachukuliwa  hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwani atakuwa amevunja sheria ya takwimu sura ya 351.
 
Alisema kuwa kwa zoezi hili serikali haitamuonea aibu mtu yeyote atakayeonekana anania ya kukwamisha zoezi hilo hivyo ni vema wale wenye mawazo hayo wakaacha mapema kwani serikali imejiandaa kukabiliana na wote wenye nia ovu kuhusu zoezi hilo .
 

No comments: