Pages

KAPIPI TV

Wednesday, June 13, 2012

YALIYOJIRI KWENYE FACEBOOK LEO

BEWARE FB hakuna Muoaji, Matapeli watupu! Dada...
Nassor Wazambi 1:42am Jun 13
BEWARE
FB hakuna Muoaji, Matapeli watupu!

"Dada mmoja mrembo wa shani (jina kapuni) ambae ni mwanafunzi wa chuo cha utumishi wa uma (UHAZILI) tawi la tabora, pia ni member mwenzetu humu ndani, amekumbana na matapeli wa mapenzi wa FACEBOOK!
 
Mrembo huyo alipata rafiki wakiume humu FB na baada ya mawasiliano ya muda mrefu wakaamua waende hatua ya pili ya mahusiano, wakakubaliana kuwa wapenzi ingawa hawakuwahi kuonana! baada ya mahusiano ya kimtandao ya muda mrefu dada yetu akajenga imani kubwa kwa njemba huyo ambaye kama kwaida alikuwa ana saidia pindi akipigwa mizinga ya hapa na pale(ATM BOXMAN) .
 
June hii wakakubaliana mrembo aende likizo aliko mpenzi huyo fake huku njemba hilo likiahidi kutuma nauli, ila akamuambia mpenzi wake amtumie picha zake akiwa mtupu (uchi)! dada wawatu akiwa hajui hili wala lile akapiga picha za uchi za kutosha akazi email kwa jamaa! kuzipata tu jamaa huyo akampigia cm akamwambia amlipe Tsh. laki sita vinginevyo anazipeleka picha hizo kwenye magazeti ya udaku! mdada akaduwaa, hela hana akaacha mambo yaende kama yalivyo.
 Jamaa alipoona dada hana kitu akaenda kuziuza picha hizo kwenye moja ya magazeti PENDWA au ya UDAKU kama ilivyozoeleka!
 
Gazeti likampigia simu  kubalance  stori, mdada wa watu akabembeleza amekubaliwa wasitoe hiyo stori ila arudishe tsh. laki 6 walizotumia kununua picha hizo! 
Inasemekana hivi sasa mdada huyo anahaha kusaka noti azime ishu!"
 
KAZI KWENU WAREMBO

No comments: