Pages

KAPIPI TV

Friday, June 1, 2012

WILAYA YA SIKONGE INAVYOTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE,MKOANI TABORA INAVYOTEKELEZA MIRADI
KADHAA YA MAENDELEO.
Mkururugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge,Paul Nkulila,alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa makala hii.

 Hastin Liumba,Sikonge
Mradi wa  ujenzi wa ofisi ya Makao Makuu ya Halmashauri wilaya ya Sikonge.

HALMASHAURI ya wilaya ya Sikonge ilianzishwa mwaka Alisema kuwa hadi
Mwaka  mwaka 1997 na hadi sasa ikiwa na tarafa 2,kata 17,vijiji 64 na
vitongoji 241 na hadi kufikia kipindi cha mwezi disemba mwaka
2011,wilaya hiyo ilikuwa na wakazi wapatao 204,453..

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Sikonge, Paul Nkulila anafanya
mazungumzo na mwandishi wa makala hii kuelezea jinsi wanavyotekeleza
miradi kadhaa ya maendeleo wilayani humo.

Nkulila anaanza kwa kuuzungumzia mradi wa ujenzi wa ofisi ya utawala
la halmashauri ya wilaya ya Sikonge ambayo, inakabiliwa na tatizo
kubwa la uhaba wa vyumba vya ofisi za idara zake, hivyo basi kwa
kushirikiana na Serikali Kuu halmashauri ilianzisha Mradi wa ujenzi wa
jengo la ofisi litakalokuwa na uwezo wa kuwa na ofisi zote za
halmashauri.

Mkurugenzi huyo anaeleza kuwa jengo hilo linalotarajiwa kuwa na
ghorofa nne nne, linakadiriwa kugharimu kiasi cha sh. 5,000,000,000/=
hadi litakapokamilika.
Anasema kwa sasa ujenzi huo umefikia hatua ya msingi na unatarajiwa
kukamilika kwa muda wa miaka mitatu, yaani mwaka 2013/2014.

Aidha anaeleza kuwa hadi sasa Serikali Kuu imeipatia Halmashauri fedha
kiasi cha sh. 1,400,000,000 za ujenzi wa jengo hilo la utawala, na
ujenzi wake unaendelea.

Nkulila alisema mradi huu ulianza kutekelezwa mei 28 mwaka 2010, mara
baada ya kuingia mkataba baina ya Halmashauri na Mhandisi Mshauri
Mekon Arch Consult Co. Ltd wa jijini Dar es Salaamu, kwa ajili ya kazi
ya kuandaa michoro, vitabu vya Zabuni na usimamizi wa kazi wakati wa
ujenzi.

Aidha anaongeza kuwa kaazi hii ya kuandaa michoro, vitabu vya Zabuni
na usimamizi wa kazi wakati wa ujenzi uligharimu kiasi cha sh. Milioni
142,050,000.00
ambazo ni ruzuku ya Serikali za mitaa kwa miradi ya Maendeleo (LGDG),
kutoka Serikali kuu ambapo hadi sasa mhandisi mshauri amelipwa sh.
42,615,000.000
Mkurugenzi huyo alisema hali ya ukosefu wa vyumba vya ofisi itafikia
mahali kero hiyo intaondoshwa kwa jengo hilo litamaliza upungufu huo.
Ujenzi wake

Aidha mkurugenzi huyo anabainisha kuwa kazi ya ujenzi wa jengo la
ofisi utajengwa katika awamu mbalimbali,ambapo awamu ya kwanza ujenzi
wake tayari umeanza na kazi amepewa mkandarasi Brave “Engineering and
Construction Comp. Ltd” ya jijini Dar es Salaamu, kwa mkataba wenye
thamani ya sh. 709,856,492.00 mkandarasi alianza ujenzi tarehe 11
Novemba 2011.

Nkulila alisema mkandarasi huyo anatakiwa kukamilisha ujenzi ndani ya
miezi tisa, kwa mujibu wa mkataba.

Alisema hadi sasa mkandarasi tayari amekwisha lipwa kiasi cha sh.
106,478,473.80 ikiwa ni malipo ya awali. Hadi sasa ujenzi upo hatua ya
msingi na ujenzi unaendelea.
“Jengo hili likikamilika litakuwa na uwezo wa kuondoa upungufu wa ofisi kwa Halmashauri kwa asilimia 100, kwa upande wa makao Makuu ya halmashauri
na kuondoa usu mbufu wote uliopo.” Anaongeza.

Aidha mkurugenzi huyo anasema kuwa ujenzi wa jengo la hilo la makao
makuu ya halmashari yake awamu ya pili unatarajiwa kuanza mwezi Julai
2012 mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa awamu ya kwanza.

Inavyokabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi wilayani.

Kuhusu upungufu uliopo wa nyumba za watumishi wa halmashauri ya wilaya
ya Sikonge, mkurugenzi huyo anaeleza kuwa halmashauri hiyo,iko
pembezoni mwa mkoa wa Tabora,na jitihada zinzfanyika kuweza kuondosha
upungufu kwa asilimia 100, wa nyumba za watumishi wanaofanya kazi
katika halmashauri hiyo.

Alisema kuwa hadi Mwaka 2011 halmashauri ilikuwa haina hata nyumba
moja ya mkuu  wa idara toka ilipoanzishwa mwaka 1997.

Aidha anaongeza kwa kushirikiana na Serikali kuu, halmashauri ya
Wilaya ya Sikonge  ilianzisha mradi ujenzi wa nyumba 10, kwa ajili ya
wakuu wa Idara ili kupunguza tatizo kubwa la nyumba za watumishi
lililopo wilayani humo.

Anaeleza kuwa ujenzi huo wa nyumba kumi,  wenye thamani ya sh
293,626,834  unajengwa na mkandarasi  Monmar & Sons wa Tabora. Ambapo
mkandarasi huyo alianza kazi hiyo rasmi mnamo mwezi  April 4, 2010, na
alikamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza mwezi juni 30, 2011.

Hata hivyo mkurugenzi huyo anasema kutokana na sababu mbalimbali kama
vile maeneo kuendelea kushikiliwa na wananchi, mkandarasi alishindwa
kuanza kazi zake za ujenzi wa majengo hayo kwa wakati ili kuwasubiri
wananchi waliokuwa wanamiliki maeneo hayo  waweze kuvuna mazao yao na
kulipwa fidia,na kazi hiyo ilianza mara moja.

Hatua iliyofikiwa awamu ya  kwanza.

Nkulila anaeleza kuwa ujenzi wa nyumba 10 awamu ya kwanza umefikia
hatua  ya nyumba 5, za kwanza ambazo hadi sasa zimekamilika hadi hatua
ya umaliziaji (Finishing) kasoro mifumo ya maji safi, maji taka na
umeme.

Aidha katika nyumba 5, zilizobaki zimekamilika hadi hatua ya
kupauliwa, kuweka fremu za madirisha na milango na maandalizi mengine
yatafuatia.

Hata hivyo kulingana na makadirio yaliyofanywa na mhandisi ujenzi
wilaya Injinia Filbert Mpalasinge alisema, awamu ya pili ya ujenzi wa
nyumba 10 za watumishi, unatarajiwa kugharimu kiasi cha sh 150,000,000
hadi kukamilika.

Aidha Nkulila anaongeza fedha hiyo imetengwa katika bajeti ya
2011/2012 na hadi sasa makisio ya kazi yameisha andaliwa, tunasubiri
mchakato wa manunuzi ili kumpata mkandarasi atakaekamilisha kazi hiyo.

Mkurugenzi huyo anaeleza zaidi kuwa licha ya nyumba  10  za wakuu wa
Idara wa halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, pia imeanza mchakato wa
ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi itakayojengwa katika eneo la Usupilo
kwa gharama ambayo itakuwa si chini ya  sh 200,000,000.

Alisema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kujengwa kwa awamu mbili,  ambapo
awamu ya kwanza ya kwanzaitakuwa ni mwaka 2012/13, na unatarajiwa
kukamilika mwaka wa fedha 2013/2014 kwa fedha za ruzuku ya maendeleo
ya H/W (CDG) na mapato ya ndani ya  halmashauri ya wilaya ya Sikonge.

Ujenzi wa hostel shule ya sekondari – Igigwa

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo anazungumzia utekelezaji wa
miradi ya maendeleo ya halmashauri yake kuwa kuna mradi wa ujenzi wa
hostel ya wanafunzi wa sekondari ya Igigwa.

Nkulila anasema kuwa katika mradi huo, serikali kuu iliipatia
halmashauri yake kiasi cha sh 220,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa
Hosteli ya wanafunzi wa kike Igigwa.

Alisema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2009/2010  kupitia ruzuku ya
maendeleo ya serikali za mitaa (LGDG), ambapo ni kwa ajili ya ujenzi
wa Bweni moja, bwalo, vyoo, na kufunga mfumo wa umeme wa mionzi ya jua
ambapo Hosteli hiyo inatarajia kuchukua wanafunzi 48, pindi ujenzi
utakapo kamilika.

Kuhusu ujenzi huu wa bweni,mkurugenzi huyo anasema bwalo na vyoo
tayari umeanza na upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa
ujenzi.

Anaeleza zaidi kuwa  kazi hii alipewa Mkandarasi Fena’s construction
Co. Ltd wa Tabora, na ujenzi wake ulianza mnamo mwezi disemba 16,mwaka
2010.

Alisema ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mnamo mwezi agosti 24,
mwaka 2012  baada ya kuongezewa muda ambapo ujenzi unatarajiwa
kugharimu sh 181,753,394.00 pamoja na VAT na hadi sasa ujenzi umefikia
hatua za umaliziaji.

Aidha anasema kuwa mfumo wa umeme wa mionzi ya jua, unatarajiwa
kufungwa mara baada ya ujenzi kukamilika, ambapo kiasi cha sh
20,000,000.00 zilitengwa kutoka katika fedha zilizotolewa kwa ajili ya
kazi hiyo.

”Hosteli hii itasaidia kupunguza tatizo la watoto kukaa mbali na eneo
la shule au kupanga mitaani hasa watoto wa kike pia itaongeza kiwango
cha ufaulu wa watoto kwani watapata muda mwingi wa kujisomea
zaidi”aliongeza

Alisema hosteli hii inatarajia kuchukua watoto kutoka vijiji sita
vinavyozunguka shule hii katika kata za Igigwa na Kisanga.

Miradi mingine ya halmashauri ya wilaya ya Sikonge

Mradi wa soko la kisasa.

Kaimu afisa mipango na mchumi wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge, S
Pondile anabainisha kuwa halmashauri yake immeanzisha mradi mwingine
ambapo inatarajia kujenga soko la kisasa litakalotoa huduma mbalimbali
za kibiashara ili kuwawezesha wananchi wake kuwapa maeneo ya kufanyia
biashara.

Pondile kuwa katika mradi huo wa soko baadhi ya majengo yatakayokuwemo
kwenye soko hili ni pamoja na maeneo ya biashara za vyakula, nyama,
samaki, bidhaa za misitu hususani asali na nta.

Alisema kuwa ofisi mbalimbali kama migahawa,na huduma za
kibenki,ambapo soko hili linatarajia kugharimu sh 3,000,000,000/= na
litajengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na halmashauri.

Ujenzi wa Stendi ya kisasa.

Kuhusu ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa,Pondile anaongeza kuwa
wilaya ya Sikonge ni mji unaokuwa kwa kasi na upo katika barabara kuu
iendayo Mbeya na Rukwa hivyo kuwa na idadi kubwa ya wananchi
wanaosafiri kwenda katika maeneo hayo.

Aidha anasema  ili kwenda Sanjari na idadi kubwa ya magari yanayopita
katika mji huo halmashauri imeweka katika mpango wake wa mwaka
2012/2013 ujenzi wa stendi ya Mabasi lakini pia eneo la kuegesha
malori na magari mengine.
Alisema mradi huo umetengewa bajeti ya sh 100,000,000 katika bajeti ya
mwaka 2012/2013.

Changamoto katika miradi husika miradi.

Kuhusu changamoto kwenye miradi anabainisha zipo chache ambazo
zimekuwa zikikwaza kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati.

Pondile anasema changamoto baadhi ni kupanda kwa gharama za vifaa vya
ujenzi,gharama ambazo zimekuwa zikipanda kila kukicha.

Anaongeza changamoto nyingine ni wananchi kutochangia katika miradi
kwa wakati na kufanya miradi mingi kutokamilika kwa wakati,na serikali
kushinwa kuleta fedha ambayo ilipitishwa kwenye bajeti husika.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge,Robert
Kamoga,alisema licha ya changamoto kadhaa,wamejipanga kama halmashauri
kukabiliana nazo.

Kamoga alisema wanatarajia kubuni miradi mingine kwani mji wa Sikonge
kwa sasa umekuwa ukitanuka sana hivyo kila jambo watalifanya kwa
wakati.

No comments: