Pages

KAPIPI TV

Friday, June 22, 2012

UCHAFU UNAVYOZIDI KUUTESA MJI WA TABORA"Hofu ya tishio la magonjwa ya mlipuko yatanda"

Eneo la barabara ya kutoka benki ya NBC kuelekea Standi mpya ya mabasi Tabora mjini,mifereji imeziba kwa uchafu.
Ikiwa ni mchana kweupe wengine wanajisaidia haja ndogo katika eneo la Standi mpya ya mabasi mjini Tabora
Biashara ya mishikaki nayo inafanyika pembezoni mwa eneo la Standi hiyo


Biashara ya maji ya kufunga nayo imekuwa ikifanyika katika mazingira hayo

Tatizo la uchafu katika mji wa Tabora bado linaendelea kushika kasi na hivyo kutishia kwa baadhi ya maeneo kujitokeza kwa magonjwa ya mlipuko.

Na mwandishi wetu Tabora.
 
Maeneo yaliyo mengi sasa mjini Tabora na viunga vyake yamekuwa yakikabiliwa tatizo hilo linalodaiwa  kuwa sugu ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya tani 58 huzalishwa kila siku kwa taka za majumbani na hata maeneo ya kufanyia biashara.

Uchunguzi wa mtandao huu umebaini kuwa hakuna amri yeyote ambayo imekuwa ikitilia mkazo juu ya udhibiti wa taka hizo zinazozalishwa kila kukicha ingawa zipo sheria ndogondogo zilizopitishwa na baraza la madiwani kufuatilia suala hilo.

Baadhi ya wananchi wakiwemo wafanyabiashara wamekuwa ni chanzo kikubwa cha uzalishaji wa taka hizo na kuziweka maeneo yasiyo stahili.

Ingawa yapo baadhi ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taka hizo lakini vifaa vivyowekwa na Halmashauri ya manispaa ya Tabora havitoshelezi kubeba taka zinazozalishwa mjini Tabora.

Aidha Halmashauri ya manispaa ya Tabora imekua ikishughulikia suala la uzoaji taka lakini bado inakabiliwa na tatizo la vifaa vya kuzolea taka hizo yakiwemo magari ambayo kwasasa yamechakaa kwa kiasi kikubwa.   

No comments: