Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai,
Na Mohammed Mhina na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi
KIGOMA ALHAMISI JUNI 7, 2012.
Mwanafunzi
mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kigadye wilaya ya
Kasulu mkoani Kigoma, Abeid Manase(8), amefariki dunia hapo hapo na
wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa
kwa mkono walilokuwa wakilichezea.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amewataja watoto
waliojeruhiwa na bomu hilo kuwa ni wanafunzi wawili wa darasa la kwanza
Tuju Seluke(7) aliyejeruhiwa tumboni na Sarah Manase(6) aliyejeruhiwa kwenye paja na mguu kulia. wote wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kigadye wilayani Kasulu.
Kamanda
huyo amewata wengine waliojeruhiwa kuwa ni watoto wadogo wenye umri wa
miaka minne kila mmoja ambao walikuwa wakichezea bomu hilo kwa pamoja
ambao ni Enjord Seluke aliyejeruhiwa kwenye sikio la upande wa kushoto na Isaka Yohana aliyejeruhiwa kwenye jicho la upande wa kushoto.
Kamanda
Kashai amesema majeruhi hao wote wamelazwa katika hospitali ya Misheni
iliyopo katika kijiji cha Shunge wilauani Kasulu kwa matibabu zaidi na
hali zao zimeelezwa kuwa zinaendelea vizuri.
Kamanda
Kashai amesema jana majira ya saa 11.00 jioni, huko katika kijiji cha
Kigadye, watoto hao walikuwa wakilichezea bomu hilo la kutupa kwa mkono
na ndipo lilipowalipukia na kumuua mwenzao na wengine hao wane
wakajeruhiwa.
Bomu hilo lilikuwa limefichwa katika moja ya bustani nyumbani kwa Bw. Ayoub James Luvahovi mkazi wa kijiji cha Kidae na likimbia mara baada ya tukio hilo na Polisi wanamsaka.
Katika
tukio linguine Kamanda Kashai amesema huko Kasulu, watu wenye silaha
wamemjeruhi kwa kumpiga risasi tumboni mfanyabiashara mmoja Bi.
Deothera Malusha(23) na baadaye kumpora shilingi 150,000 pamoja na simu
yake ya mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 55,000.
Amesema
baada ya uporaji huwo, majambazi hayo yalikimbia na kutokomea katika
msituni na majeruhi amelazwa kwenye Hospitali ya wilaya ya kasulu mkoni
Kigoma na hali yake bado sio nzuri.
Wakati
huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia wahamiaji haramu 52 kwa makosa ya kuingia na kuishi nchini bila ya kibali.
Kamanda
Kashai amesema kuwa wayuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali
walipokuwa wakifanya shughuli za uvuvi mkoani humo.
No comments:
Post a Comment