MWENYEKITI Mstaafu wa clabu ya waandishi wa habari mkoa wa Morogoro Boniventure Mtalimbo, ameviasa vyuo vya uandishi wa habari nchini, kuwa na mtaala wa masomo unaojali ulinzi na usalama kwa wandishi wanapokuwa kazi.
Rai hiyo ameitoa rai, wakati akichangia maoni kwenye warsha ya
waandishi wa habari iliyoandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania (TNGP),
yenye lengo la kuimarisha zaidi wajibu wa klabu za waandishi na redio
jamii, katika kuandika na kuripoti habari za kijinsia kama sehemu ya
kutangaza kampeni ya haki za uchumi ili rasilimali ziyanufaishe makundi yote wakati wa mchakato wa katiba mpya.
Mwandishi
Tumain Msowoya anaripoti kuwa ,Mtalimbo alisema, ikiwa mtaala huo
utaanzishwa kwenye vyuo hivyo utasaidia wanahabari kujua namna ya
kujikinga na mambo mbalimbali hatarishi wawapo kazini.
Alitolea mfano katika chaguzi zilizopita, ambapo alisema kulikuwa na ulinzi mdogo kwa wanahabari hali ambayo inahatarisha maisha yao.
Aidha
aliyaomba mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Taasisi pamoja na
wanaharakati wakishirikiana kwa pamoja kuangalia namna ya kuwapa
waandisi wa habari mafunzo ya kujilinda.
Naye Mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Mwananchi Venance
George, alishauri wanahabari kuwa na bima ya maisha ili wanapopata
matatizo ikiwemo kufariki wawapo kazini familia zao ziweze kutambuliwa
na bima ili kupata haki stahiki.
“
Tunatakiwa tuwe na bima ya afya ili hata ukiuwawa uki kiwa kazini
familia inabaki na kitu cha kuwasaidia, bila hivyo unakufa ukiwa kazini
watoto na mke wanaendelea kuteseka”
Kwa
upande wake Mwandishi wa habari wa Itv na Redio one John Chacha
aliwashauri wanahabari kuwa na kazi mbadala ikiwemo ujasiliamali badala
ya kutegemea habari pekee.
Hata
hivyo, muwezeshaji wa ,mafunzo wa wanahabari Alisema kwa kufanya hivyo
kutasaidia kukwepa kutumika na baadhi ya watu wanaotaka kunufaika kwa
kutumia kalamu zao, na baadae kuwadharau.
Na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment