Pages

KAPIPI TV

Friday, June 22, 2012

JAMHURI YAWASILISHA USHAHIDI WA UMRI WA LULU"Inadaiwa kuwa ana umri wa miaka 18"




Pichani ni msanii Elizabeth Michael 'Lulu' akishuka katika gari la Askari Magereza.
 
Na Hellen Mwango 
MAWAKILI upande wa Serikali kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii nyota Steven Kanumba (28),inayomkabili msanii wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' wamewasilisha katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam vielelezo vya kuthibitisha kwamba mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 18.


Vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani ni pamoja na CD iliyorekodi mahojiano kati ya Mtangazji, Maelezo ya kuomba hati ya kusafiria, na leseni ya udereva.
Pia umewasilisha Mahakamani hapo maelezo ya Polisi pamoja na maombi ya hati kusafiria ambapo mshtakiwa ameeleza kwamba ana umri zaidi ya miaka 18.


Keshi hiyo itasikilizwa Juni 25 mwaka huu mbele ya jaji Dk.Fauz Twaib Mahakamani hapo.
Juni 18 Mawakili wa nutetezi Peter Kibatala , Fugency Massawe na Kennedy Fungamtama waliwasilisha vielelezo kwa njia ya maandishi kupitia kiapo.Katika ushahidi uliowasilishwa na baba mzazi wa Elizabeth Michael Kimeleta ameapa kwamba binti yake hadi anatuhumiwa kufanya mauaji , umri wake ni miaka 17.


Kalugira mama Mzazi wa Lulu anadai kuwa alimzaa mtoto huyo miaka 17 iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Jijini Dar es Salaam.


Upande wa Jamhuri unaoongozwa na Wakili nwa Serikali Shadrack Kimaro .Lulu anakabiliwa na shtaka la mauaji dhidi ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu , katika eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Chanzo: http://bongoweekend.blogspot.com

No comments: