Pages

KAPIPI TV

Monday, June 18, 2012

ASKARI POLISI MUGUMU ADAIWA KUSHIRIKIANA NA MHARIFU''Huo ni mtandao wa uharifu unaodaiwa kuota mizizi kwa maeneo ya mikoa ya kanda ya ziwa



Huo ni mtandao wa uharifu

Mkazi mmoja wa kutoka Geita ambaye inasadikika kuwa na uhusiano wa uharifu  na askari polisi mmoja mwenye cheo cha koplo katika kituo cha polisi Mugumu.ambaye alimpa sare zake kupigia picha ya pasport size kwa ajili ya kufanyia uharifu ,juni 9
mwaka huu ndani ya nyumba ya kulala wageni ya FM iliyoko Mugumu mjini.

Hata hivyo mpiga picha huyo alistushwa na hali hiyo na kulazimika kutoa taarifa polisi hasa baada ya kumstukia askari huyo ambaye alifika na sare na kumkabidhi mtuhumiwa ambaye alidai anaitaka kwaajili ya kitambulisho cha kazi.

Wote walikamatwa na katika upekuzi mtuhumiwa huyo alibainika kuwa ni tapeli kwa kuwa alikutwa amekata karatasi na kuzifunga bandari juu ameweka tsh,10,000= za bandia ambazo walipanga kuzitumia kwa utapeli kwa kushirikiana na askari huyo,alipoulizwa alisema pia yeye ni mganga wa kienyeji ambaye hakuwa na leseni.

Kamanda wa polisi wilaya Pius Mboko alikiri kuwakamata na kudai kuwa katika maelezo ya askari huyo mwenye sare aliyetajwa kwa jinala Nyiti alidai kuwa walikuwa na uhusiano na mtuhumiwa huyo ambao hajautaja,na kuwa siku ya tukio mtuhumiwa huyo alichukua sare hizo na kupigia picha wakati yeye akiwa bafuni akioga,hata hivyo huyo askari haishi gesti ilikuwaje akaoge gesti na hata wakati wanakamatwa usiku walkutwa wote. 

Hata hivyo askari huyo ameachiwa kwa madai kuwa sare yake ilitumiwa na mtuhumiwa akiwa anaoga.

No comments: