Pages

KAPIPI TV

Thursday, June 14, 2012

ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMUUA MTOTO WAKE KIGOMA


Na Mohammed Mhina na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi
 Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia mkazi mmoja wa Mpeta, Sarah Dasse(23), kwa tuhuma za kumua mtoto wake aitwaye Zainabu Sita mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kwa kumkaba shingo hadi kufa.
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma  ACP Frasser Kashai amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa chanzo cha mauaji hayo na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka lake la mauaji ya kikatili.
Kuhusiana na masuala mengine ya Kiusalama, Kamanda Kashai pia amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za siri Polisi endap[o watabaini kuwepo kwa uhalifu na wahalifu ili wahusika wawekewe mitego na kutiwa mbaroni.
Wakati huo huo:-
  Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa  kijiji cha Muhunga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Vesta  Mahwa, amefariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki huko kwenye Barabara ya Lumumba eneo la Mwanga mjini Kigoma.
Kamanda Kashai, amesema kuwa ajali hiyo ilimetokea majira ya saa 12.45 jioni ya Jumapili wiki iliyopita  huko kwenye Barabara ya Lumumba Mwanga mjini Kigoma.
Amesema ajali hiyo ilitokea wakati Dereva mmoja wa bodaboda aitwaye Kayuza Mgambo(35), mkazi wa Burega mkoani Kigoma alipokuwa akiendesha pikipiki yake kwa mwendo kasi na hatimaye kumgonga mzee huyo aliyekuwa  akitembea pembeni mwa barabara.
Alisema mpitanjia huyo ambaye kwa sasa ni marehemu, alipata jelaha kubwa kichwani huku Dereva huyo wa pikipiki yeye akivunjika taya zote na kupelekea kupoteza fahamu.
Kamanda Kashai amesema mara baada ya ajali hiyo, majeruhi wote walichukuliwa kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni kwa matibabu zaidi lakini wakati madaktari walipokuwa wakiendelea kuwatibu majeruhi hao, mzee Mahwa alifariki dunia.
Hata hivyo, Kamanda Kashai amesema, dereva wa pikipiki ambaye alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa ya Maweni, hivi sasa amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza kwa matibabu zaidi ya taya zake.
Aidha Kamanda Kashai, ametoa wito kwa madereva wa pikipiki (bodaboda) kuwa  mbali ya kujiepusha na uporwaji wa pikipiki zao na wateja, lakini pia amewataka kuwa waangalifu barabarani ili wasiwe kikwazo ama kusababisha ajali kwa watumiaji wengine wa barabara.

0784 886488, 0715 886488 Insp. Mhina

No comments: