Pages

KAPIPI TV

Thursday, May 17, 2012

MKUU WA MKOA WA TABORA FATMA MWASSA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA"Wakuu wa wilaya wanawake wawataka wananchi kutovunjika moyo kwa wao kuwepo wengi Tabora"

 Mkuu wa wilaya ya Uyui Mh.Lucy Mayenga wakati akiapishwa katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Tabora.

 Mkuu wa wilaya ya Nzega Mh.Bituni Msangi wakati akiapishwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Mh.Fatma Mwassa katika hafla fupi.
 Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mh.Hanifa Mohammed wakati akila kiapo kwa ajili ya kushika wadhifa huo.

 Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Mh.Suleiman Kumchaya wakati akiapishwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Mh.Fatma Mwassa.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh.Fatma Mwassa wakati akitoa hotuba yake kwa wakuu wa wilaya mara baada ya kuwaapisha katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi uliopo ofisini kwake mjini Tabora.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora akiwa na wakuu wa wilaya zote saba za mkoa wa Tabora muda mfupi mara baada ya kuwaapisha katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.

 Kutoka kushoto ni Mbunge wa Sikonge Mh.Said Nkumba,Mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini Mh.Suma,na Meya wa manispaa ya Tabora Mh.Ghulam Dewij walipohudhuria hafla ya kiapo kwa wakuu wa wilaya saba za mkoa wa Tabora.
 Baadhi ya maafisa waliohdhuria hafla hiyo.


Na Robert Kakwesi,Tabora
wakuu wa wilaya wanawake


WAKUU wa Wilaya Wanawake Mkoani Tabora,wamewataka wananchi Mkoani Tabora,kutovunjika moyo kwa kuwepo idadi kubwa ya wakuu wa Wilaya Wanawake.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wapya mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa,Bi Fatma Mwassa,Mkuu mpya wa wilaya ya Tabora,Seleiman Kumchaya,alisema wakuu wa wilaya wamemuagiza awaeleze wananchi kuwa wao wamekuja kuchapa kazi.

Alisema ofisi zao zitakuwa wazi kwa watu wote na hawatabagua huku wakiwahimiza wananchi wasiwaogope bali wawape ushirikiano ili maendeleo yapatikane.

Bw kumchaya amesema kwa vile Mkuu wa Mkoa tayari ana sifa ya uchapa kazi wao hawakuja kumwangusha bali kumuunga mkono kwa kufanya kazi na kuahidi watachapa kazi usiku na mchana.

Wilaya ya tabora yenye wilaya saba,kati ya hizo,Tano wakuu wake wa wilaya ni wanawake ambao ni Anna Magowa(Urambo),Bituni Msangi(Nzega),Hanifa Mohamed(Sikonge),Lucy Mayenga(Uyui) na Fatuma Kimario(Igunga).

No comments: