Pages

KAPIPI TV

Monday, May 14, 2012

MADIWANI WATUNISHA MISULI-NZEGA WAMKATAA MKURUGENZI...TARIME WAMKATAA DC

 Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nzega wameazimia kumkataa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw.Kyuza Kitundu kufuatia madai kwamba mkurugenzi huyo amekuwa akizembea katika utatuzi wa masuala mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Wakiwa katika baraza hilo lililofanyika hivi karibuni madiwani hao wakati wakijadili na kuchangia hoja mbalimbali katika baraza hilo,walibaini kuwepo kwa mapungufu kadhaa katika sekta za ardhi,elimu na afya mambo ambayo ilidhihirika kuwa kumekuwepo na kasoro za kiutendaji zinazo kwamisha maendeleo.

Hata hivyo pamoja na lile la utekelezaji mbovu wa madai na haki stahili za walimu wa wilaya ya Nzega ambao wamekuwa wakidaiwa kuyumbishwa na ofisi ya mkurugenzi huyo hata kufikia hatua ya walimu wapatao 450 kuandamana,madiwani hao waliliona hilo kuwa ni kasoro kubwa ambayo itasababisha hata kushuka kwa kiwango cha elimu kwa wanafunzi kutokana na walimu kutangaza mgomo ikiwa hawatalipwa haki zao.

Mbali na suala la ubadhirifu katika idara ya ardhi,madiwani hao bado waliendelea kuonesha msimamo wao wa kumkataa mkurugenzi huyo kwa madai kuwa amekuwa akipuuza maagizo anayopewa na baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.

Wakati huo huo
Anthony Mayunga anaripoti kutoka Tarime.   

  
BARAZA la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Tarime wamemkataa
mkuu wa wilaya hiyo John Henjewelle kwa madai kuwa hafai kuendelea
kuwepo wilayani hapo kutokana na uwezo wake mdogo wa uongozi ,kwa kuwa
ameshindwa kusimamia masuala ya ulinzi na usalama.
 
Uamzi huo umekuja siku moja tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya
uteuzi wa wakuu wa wilaya na kumbakisha Henjewelle wilayani
hapo,kitendo kilichopingwa na madiwani hao wakiongozwa na mwenyekiti
wake Amos Sagara (CCM)

Wanamtuhumu kwa kushindwa kusimamia ulinzi na usalama na mauaji ya
askari dhidi ya raia katika mgodi wa African Barrick North Mara
,ambapo anatuhumiwa kuwa na maslahi binafsi mgodini hapo.

Pia matumizi mabaya ya madaraka baada ya kudaiwa kushirikiana na
wajumbe wa serikali ya kijiji cha Nyakunguru kata ya Wegita Abel Mwita
na kumwondoa kinyume cha sheria na kuweka mtu wake ,ili aweze kupewa
ardhi kijijini hapo ambapo naye ni miongoni mwa wananchi wanaodaiwa
kusubiri malipo ya fidia kutoka mgodini hapo.

Tuhuma nyingine waliyodai ni kuruhusu vizuizi vingi katika maeneo hayo
ambapo wananchi hasa wakulima wananyanyaswa kwa kudaiwa rushwa na
askari polisi huku wakiruhusu magendo.

Walibainisha kuwa alizuia mgodi wa North Mara kutokutoa fedha
zakulipia wanafunzi wa sekondari na kuhamishia utaratibu ofisini kwake
na kubainika kuwa alikuwa akichukua watoto wa marafiki zake na wengine
si wazawa wa wilaya hiyo.

Henjewelle ilidaiwa kuwa amekuwa akidharau madiwani wa viti maalum
kuwa hawana uelewa wowote,na hata alidiriki kuwaeleza viongozi wa dini
kutoka ndani na  nje ya nchi kuwa wilaya hiyo haitawaliki na kuwa
tafiti zake zilibaini kuwa hao si Wakurya wa Tanzania wala Kenya bali
ni wa Tarime tu,kwa kifupi yeye anahimaya yake.

Katika matumizi mabaya ya madaraka pia inadaiwa kumshinikiza mshauri
wa Mgambo amwondoe afisa mtendaji wa kata ya sabasaba kwenye jengo la
halmashauri kwa madai kuwa wafungue kantini yao,hata hivyo Mkurugenzi
mtendaji Fidelis Lumato amesema mtendaji hataondoka kwa kuwa jengo ni
mali ya halmshauri na yuko kihalali.

Mgogoro wa jeshi la wananchi na wananchi kuhusu ardhi ameshindwa
kutatua matokeo yake wananchi wanadaiwa kupigwa na kunyanyaswa
,kitendo wanachodai kuwa kitakuwa na madhara makubwa.

Hivyo waliamua kutofanya kikao hicho kilichokuwa maalum kwa ajili ya
kujadili taarifa ya CAG mpaka mkuu wa  mkoa awepo ili wamweleze sababu
za kumkataa na kumkabidhi aondoke naye ili akapangiwe kituo.

Walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa hawako tayari kushirikiana naye
wala maagizo ya serikali kupitia kwake hawatayatekeleza,na kuwa kwa
usalama wake anatakiwa kutoka wilaya hiyo kung'ang;ania kukaa hapo
huenda madhara makubwa yakatokea.

Hata hivyo yeye alipoulizwa alidai kuwa yeye hakujipangia kuwa hapo
bali ameteuliwa na kuwa kama ataambiwa kutoka atatoka,hata hivyo
hakuwa tayari kujibu tuhuma hizo kwa madai kuwa hawezi kueleza bali
madiwani waseme tu.

Uamzi wa madiwani umeungwa mkono na wananchi wakiwemo watumishi ambao
walidai amekuwa akiendesha wilaya kwa ubabe ambao wanadai aliuonyesha
hivi karibuni kwa kumpiga mdogo wake kwa masuala ya mirathi na anakesi
mahakamani mkoani Dar es salaam.

Madiwani wa CCM wanadai hata ndani ya chama alishaonywa kuhusiana na
mwenendo wake na kupuuza.

No comments: