Mhariri
Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto) akipokea tuzo
maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Jamhuri ya
Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo), Murat Karakaya iliyotolewa kwa
niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri
Mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada
katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu
'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro
na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo
ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa
vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Baadhi
ya washiriki wakifuatilia wakati Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo,
Willy Edward (mbele kwenye video) akiwasilisha mada katika mkutano wa
Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari
kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini
Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya
Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na
wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Profesa,
Dk. Mohamed Bakari, raia wa Kenya anayefundisha Chuo Kikuu cha Fatih
nchini Uturuki, akipokea tuzo maalumu iliyotolewa kwa niaba ya Naibu
Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc baada ya kuwasilisha mada katika
mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Afrika
ya Leo: Sera za Siasa, Uchumi na Mambo ya Nje' mjini Ankara, Uturuki
wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya
habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mkurugenzi
wa Raia Mwema aliyepata pia kuwa MhaririMtendaji wa gazeti hilo na
Kampuni ya New Habari Corporation 2006, John Bwire (kushoto) na Mhariri
wa Makala wa Habari Leo, Selemani Nzaro wakifuatilia mkutano wa Jukwaa
la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki
iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki,
ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka
nchi 54 za Afrika.
Mhariri
Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akiwasilisha mada katika
mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo
vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na
ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa
na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari
na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
No comments:
Post a Comment