Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 16, 2012

JINSI RAIA WA SUDAN KUSINI WANAVYOKABILIWA NA NJAA


Raia wa Sudan Kusini wakabiliwa na njaa
Shirika hilo limesema kuwa mapigano katika maeneo ya mipaka na pia kufungwa kwa visima kadhaa vya mafuta kumetatiza uchumi wa Sudan Kusini.
 
Ripoti hiyo inaonya kuwa kadiri machafuko yanavyoendelea kati ya Sudan na Sudan Kusini ndivyo baa la njaa linazidi kutatiza wa Sudan Kusini.
 
Hapo awali ilikadiriwa kuwa watu takriban zaidi ya milioni 4.7 walikuwa wanakabiliwa na njaa. Lakini sasa yaonekana hali ni mbaya zaidi.
 
Nchi hiyo kwa wakati huu inahitaji nafaka tani nusu milioni.
Barabara mbovu zinafanya mambo kuwa magumu zaidi kwani usambazaji wa vyakula huwa vigumu zaidi.
Chanzo:BBC

No comments: