Pages

KAPIPI TV

Monday, April 16, 2012

VIONGOZI WA CHAMA CHA MSINGI USANGANYA-SIKONGE WATISHIANA KUUANA"Wadaiwa kutumia RADI,yakosa mtu na kupasua jengo la Ofisi yao"


 Mwenyekiti wa Chama  cha Msingi Usanganya Bw.Peter Ignas akiongea na baadhi ya viongozi wenzake katika kikao cha dharura.kilichofanyika kwenye jengo la Ofisi mpya ya Chama hicho.


Viongozi wa ngazi ya juu ya Chama cha msingi Usanganya wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu ambao umefikia hatua hata ya kutishia kuuana jambo ambalo limesababisha hata baadhi ya wakulima wa tumbaku wa kijiji cha Usanganya kuwa na mashaka ya kuuzia tumbaku yao katika chama hicho.


Mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Peter Ignas kufuatia hali hiyo inayoendelea kusababisha mtafaruku mkubwa miongoni mwa viongozi na hata kwa wanachama wa chama hicho ambao kimsingi ni wakulima wa zao la tumbaku,amelazimika kuitisha kikao cha dharura ikiwa ni hatua nyingine ya kutangaza vitisho vya mauaji alivyopatiwa hivi karibuni na baadhi ya viongozi wenzake.

Sambamba na hilo Bw.Ignas ambaye pia alikuwa akishutumiwa na baadhi ya viongozi wenzake kutumia madaraka yake vibaya ikiwa ni pamoja na kutowashirikisha viongozi wenzake katika maamuzi mbalimbali yanayohusu Chama hicho cha msingi,alibainisha katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na waandishi wa habari kama wageni waalikwa kuwa tayari vitisho dhidi yake amekwisha toa taarifa kwenye vyombo vya usalama na kuwataja mjajina halisi viongozi ambao wanaohusika na hilo.

Hata hivyo kwa upande mwingine kikao hicho kilichochukua zaidi ya saa mbili kilitawaliwa na imani za kishirikiana kufuatia Radi kupiga jengo hilo jipya la Ofisi ya chama hicho na kuharibu madirisha na sakafu siku moja kabla ya kufanyika kwa kikao hicho.

Tukio hilo pia limeendelea kujenga hofu kubwa hata kwa baadhi ya wanachama zaidi ya 85 wanaodai kwa chama hicho cha msingi malipo ya mauzo ya tumbaku kwa zaidi ya dola za kimarekani  28 elfu.

Kwaupande mwingine wanachama wa chama hicho huenda wakaacha kuuzia tumbaku yao katika  chama hicho kufuatia mizozo inayoendelea kurindima ambayo inahusishwa zaidi kutaka kumvua madaraka mwenyekiti wa chama hicho Bw.Peter Ignas kwa tuhuma za ufisadi.  
   

 










No comments: