Pages

KAPIPI TV

Monday, April 16, 2012

MAANDALIZI SENSA YA WATU NA MAKAZI YAANZA RASMI"Elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa Sensa"

Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa,kulia ni mkurugenzi mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa na katikati ni Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho Said,wakati walipofika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora kutambulisha utaratibu na maandalizi ya Sensa kwa mwaka 2012.
 Pichani:Kuonyesha maandalizi ya Sensa yameanza rasmi ambayo yanatajwa kuwa kwa mwaka huu itafanyika kisayansi na kwa uangalifu mkubwa.


SENSA itafanyika tarehe 26 Agosti mwaka 2012 ambayo ni miaka kumi baada ya Sensa ya mwisho ya mwaka 2002.Hii itakuwa ni Sensa ya tano tangu Tanzania kupata Uhuru.Sensa zilizotangulia zilifanyika katika miaka ya 1967,1978,1988 na 2002. 

 





No comments: