Wachezaji wa timu za michezo mbalimbali wa chuo cha Utumishi wa Umma nchini tawi la Tabora wamerejea rasmi Tabora baada ya kujipatia ushindi na kutwaa vikombe vinne kwa michezo ya mpira wa miguu,mpira wa pete na mpira wa kikapu.
Katika mashindano yaliyovishirikisha vyuo vyote vya Utumishi wa Umma nchini ambayo yamefanyika mjini Tanga,timu za kikosi cha Tabora mbali na kutwaa vikombe hivyo zimejinasibu katika mtandao huu kuwa wachezaji wake walikuwa na maandalizi mazuri na hata kufikia hatua ya kufanikisha ushindi huo mnono.
Akizungumza na waandishi wa habari chuo hapo wakati wa mapokezi ya kikosi cha timu hizo,kaimu mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora(TPSC) Hussein Lufunyo,mbali na kuwapongeza wachezaji hao kwa kukiletea heshima chuo hicho lakini alizungumzia umuhimu wa michezo hiyo kwa vyuo vinavyomilikiwa na TPSC kuwa ni sehemu ya kujenga udugu baina ya wanafunzi wa vyuo hivyo.
No comments:
Post a Comment