Pages

KAPIPI TV

Friday, April 27, 2012

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAM CHATOA TAMKO LA KUMTAKA RAIS KUWAWAJIBISHA MAWAZIRI WABADHIRIFU.


Mkurugenzi  Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Hellen Kijo BisImba (kulia) akitoa tamko leo asubuhi  jijini Dar es Salaam juu ya  kituo hicho kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mawaziri wabadhirifu wa fedha za umma.


Kituo  cha  Sheria na Haki za Binandamu kimetoa  wito kwa Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda na  Mawaziri wabadilifu wa fedha za umma.

Aidha Kituo hicho kimewataka Rais Kikwete kuwachukulia hatua za kisheria mawaziri wabadhirifu na watendaji wote wabadhirifu wa fedha za umma na kuwafilisi fedha za umma walizokwapua

Kituo hicho cha LHRC kimewataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda  na mawaziri wabadhilifu wa fedha za umma kujiuzuru wenyewe kwa maslahi ya taifa.

Akisoma taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk. Helen Kijo Bisimba amesema kuwa  Kituo kilifuatilia kwa makini mwenendo  wa bunge na kugundua kuwa wabunge wengi walikuwa na moyo  na dhamira ya dhati ya kutaka kuwajibisha serikali kwa kutaka kupiga kura ya kutokuwa  na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutokana na utendaji mbovu wa serikali.

Dk. Bisimba amesema kuwa kituo hicho kimemtaka Spika wa Bunge Anna Makinda kuitisha Bunge  katika siku kumi na nne zijazo ili ombi la wabunge lifanyike kutaka kupiga kura za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Ameongeza kuwa kuacha kufanya hivyo ilikuwa ni dharau kwa wabunge ambao ni wawakilsihi wa watanzania.

Kituo pia kimetoa wito kwa wananchi kuchukua hatua katika jambo hilo la kuwawasilisha mawaziri na watendaji wabadilifu wa fedha za umma  kwa kufuata katiba ya Nchi kama inavyoeleza katika Ibara ya 8.

Kwa mujibu wa Dk. Bisimba Ibara ya 8 ya Katiba ya Nchi inawapa nguvu wananchi kuiwajibisha serikali ikiwezekana hata kunyanyuka na kuchukua hatua  ili kujikomboa  kutoka katika dimbwi kubwa la umaskini  kutokana na kuendelea kufujisha  fedha za umma

Kituo hicho kimewaomba  wananchi kuwa wakati wito wa kuinuka utakapotelewa, basi wananchi wasisite kuchukua jukumu la  kushinikiza serikali iwajibike ipasavyo.

No comments: