Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal,akisoma hotuba yake wakati wa Kilele cha sherehe za maadhimisho
ya Siku ya Malaria Duniani, zilizofanyika leo Aprili 25, 2012 katika
Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika sherehe hizo pia
Makamu wa Rais alizindua Ripoti ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria
Tanzania Bara
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe, kuzindua Ripoti ya Mafanikio ya Utekelezaji wa Mikakati
ya Malaria kwa upande wa Tanzania Bara, wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Malaria Duniani zilizofanyika kwenye
Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo Aprili 25, 2012. Katikati
ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda (wapili kushoto) ni
Kaimu mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala, Jordan Lugwimbana.
Picha na Muhidin SUfiani-OMR
No comments:
Post a Comment