Pages

KAPIPI TV

Thursday, April 19, 2012

AIRTEL YAKIFADHIRI CHUO KIKUU CHA DODOMA KOMPYUTA NA VITABU VYA SHILINGI MIL.25


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi baadhi ya
vitabu  vya chuo kikuu vilizotolewa na Airtel kwa chuo kukuu cha Dodoma
(UDOM) kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) jana
wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo.  anaeshuhudia
ni Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa vitabu 104
na computer 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS ikiwa ni
muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Mkuu wa wilaya ya Bhahi Mheshimiwa Betty Mkwasa akiongea na waandishi wa
habari na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho jana wakati wa hafla fupi ya
makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni
25/- TZS  toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya
Elimu nchini. Anaefuata ni Makamu mkuu wa chuo hicho profesa idrisa Kikula
na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM)  Profesa Idrisa Kikula (kulia)
akiwashukuru Airtel mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya wanafunzi wa
chuo hicho jana wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na
kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS  kutoka Airtel ikiwa
ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini. Kulia ni mkuu wa
wa wilaya ya Bhahi Betty Mkwasa na toka shoto ni  Meneja Uhusiano wa Airtel
Jackson Mmbando.
Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa, akiwa na Makamu Mkuu wa chuo cha
Dodoma (UDOM) jana pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi
wa IT chuoni hapo wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel
kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na
kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS  toka Airtel ikiwa ni
muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.
 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote
vyenye thamani ya milioni 25/- TZS kwa chuo kikuu cha Dodoma ikiwa ni
muendelezo wa shughuli zake za kijamii  katika kuchangia sekta ya Elimu
nchini.

Komputa hizo pamoja na vitabu  vimekabidhiwa  kwa Makamu Mkuu wa chuo cha
UDOM kilichopo mkoani Dodoma jana wakati wa hafla fupi iliyofanyika ukumbi
mdogo wa mikutano chuoni hapo na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Bhahi Mh,
Betty Mkwasa

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya wa Bhahi aliishukuru
Airtel Tanzania kutokana na jitihada zake za kushirikiana na serikali
katika kusaidia sekta mbali mbalimbali ikiwemo elimu

 “Hili ni tukio muhimu sana mnalofanya Airtel na  inaonesha dhahiri dhamira
yenu ya kushirikiana na serikali yetu na jamii kwa ujumla kuchangia elimu
ili kuinua kiwango cha elimu nchini, hivyo kufanya hivi nchi yetu
inafaidika sana”

“ninawaomba wanafunzi kuhakikisha mnavitumia kikamilifu kompyuta na vitabu
hivi ili kujiongezea ujuzi na uelewa zaidi katika masomo kwa manufaa yenu
na  kwa taifa pia” alimaliza kusema Mh Mkwasa

Nae  Meneja uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema”  Airtel chini ya
mpango wetu maaalum wa kuchangia elimu bado tutaendelea kuchangia  elimu
nchini, leo tunaona fahari sana kuweza kujitolea sehemu ya faida yetu pia
kwa taasisi ya elimu ya juu (UDOM),  msaada wetu huu wa kompyta 20 na
vitabu 104 vya elimu ya juu ni muendelezo wa mpango wetu wa *Airtel Shule
Yetu *uliodumu kwa zaidi ya miaka saba ukiwa ni maalum kwa kuchangia elimu

 “kwa kupitia mpango wa Airtel Shule yetu  tumeshanikiwa kuzifikia zaidi ya
shule 800 na kutoa msaada wa vitabu na vifaa vya kufundishia yakiwemo pia
madawati”

Kwa mwaka 2012-2013  bado Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia
sekta ya elimu katika nyanja tofauti ikiwapo; kutoa madawati kwa shule za
msingi na sekondari, kurekebisha majengo ya shule, kutoa computer kwa shule
za sekondari na vyuo lengo hasa likiwa ni kushirikiana na serikali katika
kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu bora ili kuweza kupata nguvu kazi
ya kesho na kulikomboa taifa katika swala la umaskini na elimu duni.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM)  Profesa Idrisa Kikula
aliishukuru Airtel na kuongeza kuwa msaada huo wa kompyuta na vitabu
umeenda wakati muafaka na unahitajika sana.

“Vitabu na komputa hizi ni muhimu kwa chuo kikuu chetu cha Dodoma,
tunaamini kabisa vitabu hivi  vitasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba
wa vitabu na zaidi kuwapatia wanafunzi na walimu nyenzo za kujisomea na
kufundishia pia” alisema Profesa Idrisa Kikula Makamu mkuu wa chuo UDOM



 “Msaada huu umekuja muda muafaka kwa kuwa Komputa ni muhimu sana kwa elimu
ya juu ukizingatia karne hii ya sayansi na teknololojia  hivyo zitatumika
kufundishia masomo mbalimbali ya ICT na kuwapa wanafunzi ujuzi wa
teknolojia ya habari na sayansi ya kompyuta” alimaliza kwa kusema Profesa
Idrisa Kikula Makamu mkuu wa chuo UDOM

Chuo kikuu cha Dodoma ambacho ni maarufu kama UDOM kilifunguliwa rasmi
mwaka 2007 huku kikiwa  na sifa ya kuwa na maabara kubwa (library) kuliko
chuo chochote cha elimu ya juu kilichopo nchini. Kwa sasa chuo hicho
kinakadiriwa kuhudumia zaidi ya wafunzi 20,000 nchini huku matarajio ni
kufikisha wanafunzi kutoa elimu kwa wanafunzi 40,000 kwa siku zijazo.

No comments: