Pages

KAPIPI TV

Monday, March 19, 2012

RC FATMA MWASSA AWAONYA POLISI"Ni wale wanaowaonea raia,...Amuagiza RPC kuwafukuza kazi wanapobainika"





Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa amemuagiza kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Acp Athony Rutha kuwashughulikia baadhi ya askari Polisi wanaodaiwa kwenda kinyume na maadili ya kazi zao na hasa wale wanaowaonea raia kwa kuwapiga na hata kuwabambikizia makosa.

Aliyasema hayo hivi karibuni katika sherehe fupi ya kutoa tuzo na vyeti kwa askari Polisi waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka 2011,sherehe ambayo ilifanyika katika uwanja wa FFU Tabora.

Bi Fatma pamoja na kutoa pongezi kwa jeshi la Polisi kwa kupambana na vitendo vya uharifu ambavyo vimekuwa vikitishia amani kwa wananchi na mali zao,alisema kuna haja kwa uongozi wa jeshi hilo kuwadhibiti baadhi ya askari Polisi wanaokiuka maadili hatua ambayo itaendelea kuliimarisha na kujenga utumishi uliotukuka kwa jeshi la Polisi.

''Rpc napenda nikuagize askari yeyote anayekwenda kinyume na maadili ya kazi najua wewe unaweza kumalizana nao muondoshe akafanye kazi nyingine huko mitaani,maana hatuwezi kuwa na watu ambao wanatuchafulia heshima ya Jeshi letu"alisema mkuu huyo wa mkoa..

Kwaupande mwingine Bi.Fatma Mwassa akazungumzia matukio ya mauaji mbalimbali yanaoendelea kutokea mkoani Tabora ambapo hadi sasa hali imekuwa si ya kuridhisha.

Akitolea mfano matukio hayo ya mauaji alisema tangu Julai hadi Septemba mwaka 2011 zaidi ya vifo 53 vya  mauaji ya aina mbalimbali yalitokea na huku akiringanisha na mauaji ambayo yameendelea kutokea hivi karibuni na kuhusisha baadhi ya wazee vikongwe na viongozi ambao wameuawa kwa kupigwa risasi.

Aidha akisisitizia kuwataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na vitendo hivyo vya mauaji,mkuu huyo wa mkoa amelazimika kutangaza hadharani kwa mtu yeyote awe askari au raia atakaye wezesha kutoa taarifa za mipango ya mauji na ikafanikiwa kuzuiliwa mapema na mamlaka husika atapata zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja.

Kwaupande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Athony Rutha alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika jeshi hilo lakini bado linakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya kuwepo kwa matukio ya kujichukulia sheria mkononi na kusababisha mauaji kutokana na imani za kishirikina,wizi wa mifugo na ajali za barabarani.

Kamanda Rutha pia alizitaja changamoto zingine ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa upungufu wa vitendea kazi kama mafuta kwa ajili ya vyombo vya usafiri na kuwepo kwa uzagaaji wa silaha haramu zinazochangia ongezeko la vitendo vya ujambazi mkoani Tabora.   

Aidha katika hafla hiyo pia ambayo iliandaliwa na uongozi wa  Jeshi la Polisi mkoani Tabora sambamba na tuzo kwa askari polisi hao baadhi ya wafanyabisha wa mjini Tabora pamoja na waandishi watatu wa habari walipata tuzo ya vyeti.  









No comments: