Mkaguzi wa kituo cha Reli Ipala katika reli ya kutoka Tabora kuelekea Mwanza Bw.Gester Benjamin Byarugaba(39)amekatwa mapanga maeneo mbalimbali ya mwili wake kufuatia tukio la yeye kuwakataza baadhi ya wafugaji wa eneo la Ipala kupitisha mifugo yao kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria.
Akielezea mkasa huo katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete mmoja wa watu waliomfikisha mkaguzi huyo hospitalini hapo kwa lengo la kuokoa maisha yake, alisema baada ya Bw.Byarugaba kuwakataza wafugaji hao ambao ni vijana wawili walipinga agizo hilo na kuanza kumshambulia kwa upanga na fimbo hali iliyosababisha aanguke chini na kupoteza fahamu kwa muda.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka eneo la tukio mkaguzi huyo Bw.Byarugaba alichukuliwa baada ya kupata msaada kutoka kwa raia mwema aliyekuwa akipita katika eneo hilo ikiwa kilomita kadhaa kutoka kituo cha reli cha Ipala wilayani Nzega.
Hata hivyo mkaguzi huyo akiongea na mtandao huu kwa shida akiwa hospitalini hapo,alisema jambo kubwa zaidi lililomfanya hadi kupata kipigo hicho ni kutokana na hatua ya yeye kutekeleza majukumu yake kwakuwa wafugaji hao ni miongoni mwa watu wanaojihusisha na vitendo vya kufungua taluma na reli ili kuangusha Treni ya mizigo kwa lengo la kutaka kuiba kilichomo ndani ya mabehewa.
Pamoja na kuwa na hali isiyoridhisha kwa mkaguzi huyo kutokana na majeraha aliyoyapata kichwani,sikio la kushoto na begani alimtaja mmiliki wa mifugo hiyo ambayo vijana wake ndio waliomshambulia kuwa ni Mzee Mang'ombe wa eneo la kijiji cha Ipala.
Hata hivyo hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika na watuhumiwa wanaendelea na shughuli zao huku mkaguzi huyo akiwa na hali mbaya hospitalini.

No comments:
Post a Comment