Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 20, 2012

MAITI YA MTOTO WA MIAKA TISA YAKUTWA KWENYE MFEREJI WA MAJI MACHAFU"Inasemekana huenda kifo chake kimesababiswa na mvua kubwa wakati akienda Shuleni"

Maiti ya mtoto mdogo aliyefahamika kwa jina la Zainabu Ramadhani(9)mkazi wa kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora imeokotwa leo katika mfereji mkubwa wa maji unaotambulika kuwa ni mfereji wa Kazembe.

Mtoto huyo aliyekutwa amevalia sare ya shule ya Chekechea ya Kanyenye,sketi nyesi na blauzi nyeupe juu yake akiwa amevaa sweta la rangi ya bluu,inasemekana kuwa alikuwa anatafutwa na Mama yake mzazi tangu jana alipoondoka kwenda shule bila kurejea nyumbani.

Mwanaume mmoja aliyejihamisha kwa jina la Hamisi Mrisho alisema kuwa mtoto huyo ni mtoto wa shemeji yake na amekuwa akitafutwa tangu jana na tayari walikuwa wamekwisha toa taarifa Polisi na baadhi ya vyombo vya habari lakini hakukuwa na mafanikio yeyote ya kupatikana kwake.

Alisema leo wakati wanaendelea na jitihada za kumtafuta mtoto Zainabu,walisikia kuwa kuna maiti ya mtoto imeonekana katika mfereji wa Kazembe ulioko maeneo ya Kanyenye na mara baada ya kufika walimtambua kuwa alikuwa ni Zainabu mwenyewe.

Hata hivyo maelezo ya baadhi ya watu wakati wakiongea na mtandao huu walisema kuwa huenda kifo chake kimesababishwa na mvua kubwa iliyoanza kunyesha jana ikiambatana na radi kali kuanzia majira ya saa tatu asubuhi hadi saa nne na dakika arobaini na tano.

 Kwaupande mwingine waliielezea mvua hiyo huenda hata ingeweza kusababisha maafa kwa mtu mwenye umri mkubwa huku wakitolea mfano kwa maeneo ya kata ya Malolo ambapo mvua hiyo pia ilisababisha baadhi ya nyumba kujaa maji na wahusika kutafuta maeneo mengine ya kujisitiri.   

Aidha askari wa jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuchukua maiti ya mtoto huyo na kuipeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.


No comments: