Dereva wa Bodaboda wa kituo cha Zebra Bar manispaa ya Tabora amejikuta katika hali asiyoitarajia baada ya kununuliwa bia na mmoja wa wateja wake ambaye ni mkulima wa zao la tumbaku,dereva huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja inasemekana alikunywa bia nyingi kuliko uwezo wake.
Mtandao huu ulipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa baadhi ya watu na kumkuta dereva huyo akiwa hoi hajitambui huku hata pikipiki yake pia ilikuwa haifahamiki mahali ilipo.
Hata hivyo mmoja wa wakulima wa tumbaku ambaye naye alikuwa akipata kinywaji katika bar ya Zebra ambako ndiko tukio hilo lilitokea aliyefahamika kwa jina la Bw.Ilamata ambaye pia ni diwani wa Uyui alilazimika kukodi usafiri wa taxi ili kumpeleka nyumbani kwake dereva huyo maeneo ya kata ya Ipuli Manispaa ya Tabora.
Baadhi ya watu wamehoji kuwa hatua ya dereva huyo kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yake na hata ni hatari kwa wateja ambao anaowapata ukiachilia mbali usalama wa mali ambayo ni pikipiki anayoitumia.
Kwaupande mwingine baadhi yao walisema hata matukio ya kutekwa kwa madereva wa Bodaboda na kunyang'anywa pikipiki zao wakati mwingine wanayasababisha wao wenyewe kwa kupenda vya bure.

No comments:
Post a Comment