Pages

KAPIPI TV

Tuesday, May 8, 2012

MAKAMU WA RAIS DK.BILALI AWASILI MKOANI TABORA JIONI HII

Makamu wa Rais Dk.Ghalib Bilali mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Tabora ambapo alilakiwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa pamoja na mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Chang'a.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akiwa na baadhi ya viongozi kutoka ofisi ya Takwimu makao makuu Dar-es-salaam wakisubiri kumpokea makamu wa Rais Dk.Bilali katika uwanja wa ndege wa Tabora.
Makamu wa Rais Dk.Bilali akiangalia vikundi vya ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Tabora.
Makamu wa Rais Dk.Bilali baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Tabora leo hii jioni
Baadhi ya viongozi wa dini,Chama cha Mapinduzi na wataalamu kutoka ofisi ya Takwimu makao makuu Dar-es-salaam wakiwa ikulu ndogo ya Tabora baada ya mapokezi ya Makamu wa Rais Dk.Bilali
 Makamu wa Rais Dk.Ghalib Bilali akiteta jambo na Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa muda mfupi mara baada ya kuwasili ikulu ndogo ya Tabora leo hii jioni.
Na Juma kapipi-Tabora

Makamu wa Rais Dk.Ghalib Bilali amewasili jioni hii mjini Tabora na kulakiwa na mwenyeji wake mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa na baadhi ya viongozi mbalimbali wa dini na vyama vya siasa mkoani hapa.

Aidha kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora,makamu wa Rais atafanya ziara ya kikazi kwa muda wa siku mbili mkoani hapa ambapo moja ya shughuli kubwa atakayoifanya ni kufunga maandalizi ya awamu ya kwanza ya Sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2012.

Hafla ya kufunga maandalizi hayo ya Sensa itafanyika katika viwanja vya Chipukizi mjini hapa ambapo shughuli hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa mbili asubuhi ya kesho.

 





No comments: