Pages

KAPIPI TV

Thursday, March 9, 2017

EfG YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SOKO LA TEMEKE STERIO JIJINI DAR ES SALAAM


 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na shirika hilo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
 Mjumbe wa Bodi ya EfG, akizungumza katika maadhimisho hayo.
 Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris akitoa hutuba 
yake kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia Kituo cha Polisi Chang'ombe, Mkaguzi wa Polisi, Meshack Mpwage, akihutubia kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa muda wa wanawake wajasiriamali masokoni, Betty Mtewele na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris.
 Kikundi cha Sanaa cha Machozi kikitoa burudani.
 Waananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea. wanawake wakiwa na mabango yenye maneno ya nafaa kuwa kiongozi.
 Meza kuu.
 Wafanyabiashara katika soko la Temeke Sterio wakifuatilia maadhimisho hayo.
 Burudani za sarakasi zikiendelea.

 Nifuraha tupu katika maadhimisho hayo.
 Hapa ni kuserebuka kwa kwenda mbele 'kweli ni wanawake na maendeleo'
 Vipeperushi juu.


Wasaidizi wa kisheria katika soko la Tabata Muslim jijini Dar es Salaam, Aisha Juma (kushoto) na Irene Daniel wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Na Dotto Mwaibale

TANZANIA ya Viwanda haitawezekana bila ya kuwepo wanawake wachapa kazi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita wakati akizungumza 
na waandisi wa habari kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Soko la 
Temeke Sterio Dar es Salaam.

Magigita alisema wanawake waliowengi ndio wanaoinua uchumi wa nchi kutokana na kujikita katika ujasiriamali hivyo bila ya 
kuwepo mpango mzima wa Tanzania ya Viwanda hautakuwepo. 

Alisema wanawake wanapaswa kuendelea na sera yao ya kuhamasishana na kuunda vikundi ili iwe rahisi kwao kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka katika Taasisi za 
kifedha ili waweze kusonga mbele katika shughuli zao za ujasiriamali.

"Tunaiomba serikali katika bajeti zake itenge fungu maalumu kwa ajili ya wanawake" alisema Magigita.

Alisema kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka huu ni Tanzania ya Viwanda Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Uchumi.


Akizungumza kwa niaba ya Kamnada wa Polisi Mkoa wa Temeke, Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Mkaguzi wa Polisi, 
Meshack Mpwage alisema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na vitendo vya ukati wa kijinsia masokoni na maeneo mengine.

"Jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia tutaendelea kutoa ushirikiano na masuala yote yanyohusu ukatili wa kijinsia na hatutasita kumchukua hatua mkosaji" alisma Mpwage.

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris alisema ukatili wa kijinsia upo duniani kote na si Tanzania pekee na umekuwa ukipingwa kwa nguvu zote.

"Matukio ya ukatili wa kijinsia yapo karibu duniani kote na yamekuwa yakipgiwa kelele kutoka na ukubwa wake hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwa katika mapambano 

hayo" alisema Morris. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: