Pages

KAPIPI TV

Tuesday, January 12, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA JENGO LA ZAHANATI YA MPINGI WILAYA YA SONGEA

images
Na Mwandishi Maalum
WAZIRI WA AFYA Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mifuko ya afya Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na Halmashauri na wananchi, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.

No comments: