Pages

KAPIPI TV

Sunday, September 20, 2015

WATOTO WENYE ASILI YA KITANZANIA WANYAKUA VIKOMBE KATIKA SETLC FALL JR. OPEN 2015 WASHINGTON,DC.

Vijana wenye asili ya Kitanzania Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki wameonyesha umahiri wa mchezo wa Tennis uliofanyika  Jumamosi, September 19,2015 katika viwanja vya nyumbani kwao South East Tennis and Learning Center, South East Washington, DC.
Briana Kagemuro alikuwa katika kinyanganyiro cha Wasichana wenye umri wa miaka 12 Singles (Girls 12 singles) ambapo alimshida Isabella De Leo 6-4,6-4; Cassi Chen 7-6,6-3,10-6 na Asha verma 6-4,6-4.

Naye Bryan Mwombeki alipata kombe lake la ushindi la wavulana wenye umri wa miaka 10 (USTA) (Boy's 10 Singles) dhidi ya Jason De Silva 4-0,4-0, Arbert Vardimisky 4-3,4-1; Aarush Rajanala 4-1,4-2.

Bryan Mwombeki


Briana Kagemuro

Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao wa mchezo huo mapema leo siku ya Jumamosi Septemba 19, 2015 baada ya kushinda makombe yao.

No comments: