![]() |
| Mke wa Mgombea ubunge wa jimbo la Mpanda Mjini Bi Josephine Rupia akiwasalimia wananchi na kumwombea kura mmewe katika mkutano huo wa Kampeni |
Na KIBADA
Mgombea Ubunge kwa tikekti ya CCM Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Simon Kapufi amesema iwapo atapatiwa ridhaa na wananchi kuwa mwakilishi wao kwa nafasi ya mbunge atashirikiana,na wananchi, madiwani na watalaam kwenye Halmashauri pamoja na Wadau wa kuhakikisha wanaleta maendeleo.
Kapufi amesisitiza kuwa elimu itakuwa ni kipaumbele chake cha kwanza na iwapo atapatiwa nafasi ya uwakilishi tajitahidi kushughulikia suala la uhaba wa madawati,mashuleni na tatizo la chakula kwa wanafunzi mashuleni, pia atakuwa mbunifu kwa kubuni miradi itakayosaidia kuwaunganisha makundi ya vijana akina mama na wajasilia mali kuanzisha miradi ya ujasiliamali ili kuondokana na umasikini.
Awali Katibu wa CCM Mkoa wa KATAVI Avelin Mushi akaaeleza kuwa kiongozi bora ni Yule asiyewagawa wananchi katika kuleta maendeleo,akakemea suala la udini,ukabila na ukanda kuwa suala hilo halina nafasi katika siasa za nchi hii,viongozi wa namna hiyo hawafai kupewa uongozi wananchi wajiepushe nao.
Awaomba wananchi wachague chamacha Mapinduzi ili kuleta maendeleo ya haraka nay a kweli.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Abdalah Mselem kizungumza katika Mkutano huo amewataka wananchi kuchagua wagombea kutoka CCM kwa kuwa ndiyo chama pekee kitakachoendelea kuwaletea maendeleo na kudumisha amani ya nchi hii.
Mselem akatatumia mkutano huo kuwaomba wale waliokihama chama hicho kutokana na kukosa nafasi baada ya kura za maoni kutotosha wasihame badala yaka kama walikuwa wamekihama wareje waje wajengee chama na wale wa upande wapili akawaomba kura zao zote wakipigie chama cha mapinduzi na kisha warejea kwenye chama hicho waendelee kukijenga kwa kuwa waliokosa kura za maoni isiwe sababu ya kuhama cha hata wakiwa nje ya CCM hawawezi kupta mafanikio ni vyema wakarudi CCM.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda Beda Katani amewaasa wananchi kukichagua chama cha mapinduzi kuhakikisha kinaendelea kuongoza kwa kuwa jimbo la mpanda mjini limepotea mikono mwa wapinzani kwa kipindi cha miaka kumi hivyo wanahitaji wananchi maendeleo ya dhati.






No comments:
Post a Comment