Na Mwandishi wetu
OFISA
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP na Mbunge wa Singida Mjini kupitia tiketi
ya CCM, Mohammed Dewji, amesema kazi ya kutengeneza utajiri sio rahisi,
inahitaji mipangilio madhubuti na uvumilivu ili kufanikisha lengo hilo.
Mbunge
huyo ambaye kampuni zake zimeajiri watu 24,000 sawa na asilimia 5 ya
ajira rasmi nchini, amesema kutengeneza utajiri hakufanyiki kwa njia ya
kupanda lifti bali ni ujenzi wa tofali kwa tofali hadi nyumba
kukamilika.
Akiwa
anaendesha kampuni ambayo pato lake hadi mwishoni mwa mwaka huu
litakuwa ni za Marekani bilioni 1.5 amesema uwezo huo haukupatikana mara
moja bali umetokana na nia pamoja na kutrumia vyema fursa
zinazopatikana nchini.
Amesema
katika uzinduzi wa Jarida la IRIS Executive linalomilikiwa na Kituo cha
Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambacho kina ofisi
Tanzania, Kenya na wawakilishi nchini Uganda na Rwanda Vijana wa
Tanzania wapo katika nchi inayofaa na wakati muafaka na hivyo wanauwezo
mkubwa wa kutoka kiuuchumi.
Alisema
wakati uchumi wa afrika unakua kwa asilimia 5 na wa dunia kwa asilimia 8
uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 hali inayotoa nafasi kubwa kwa
vijana kusonga mbele ili mradi wachapekazi kwa bidii na maarifa.
Katika
uzinduzi wa jarida hilo lenye nakala 40,000 mtaani katika nchi zote za
Afrika Mashariki na likizingatia mahitaji ya ukuaji wa uchumi Afrika
Mashariki, Dewji maarufu kama Mo amewataka vijana kuhakikisha kwamba
wanatoa habari kwa haraka na kwa muda muafaka kwani ndio kichochea cha
uwekezaji na uendeshaji.
Alikubaliana
na Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo Mike Mina kwamba habari ni kitu
muhimu katika kufanikisha uwekezaji na biashara, lakini akasisitiza
habari zinaoztolewa katika muda muafaka.
IRIS
Executive ambalo katika toleo lake la pili limeandika habari kumhusu Mo
ambaye kwa miaka 15 amefanikiwa kuiondoa MeTL kutoka pato la dola
milioni 30 hadi dola bilioni 1.5,huandika na kufuatilia masuala ya
maendeleo hasa katika sekta zinazogusa uchumi moja kwa moja kama fedha
na benki, uzalishaji viwandani, mafuta na gesi, kilimo na uwekezaji.
Toleo lake la kwanza lilimgusa Ofisa Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi.
Akizungumza
historia yake kabla ya kuzindua jarida hilo alisema kwamba yeye
alizaliwa nyumbani na mkunga wa kienyeji 1975 kama walivyo watanzania
wengi na kwamba amefikia hapo kwa bidii kubwa akitaka vijana kuiga
safari hiyo kwa kutumia vyema fursa zilizopo.
Kampuni
ya MeTL inafanya shughuli anuai kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo
na viwanda, lojistiki, huduma za fedha,majumba ya biashara,
petroli,vinu vya kusindika nafaka,vifaa vya plastiki, usambazaji na
masuala ya simu.
Aidha
kampuni hiyo inajivunia kufanya biashara katika nchi za Ethiopia,
Malawi, Msumbiji, Zambia, Dubai, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudan
Kusini na Kenya huku ikiwa na viwanda zaidi ya 31 nchini Tanzania pekee.
Dewji
amepata elimu ya juu kutoka Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani
ambacho katika baadhi ya maelezo yake anasema ndio iliyomfumbua macho na
kuona umuhimu wa kutumia fursa za ushindani wa kibiashara duniani.
Mara
nyingi MO amekuwa akisema,Falsafa yake kama mfanyabiashara sio kuridhika
na mafanikio aliyonayo bali kuendelea kufanyakazi kwa bidii na
kufanikiwa zaidi. Alisema.
Naye
Ofisa Mtendaji Mkuu- IRIS Executive Development Center, Phylisiah Mcheni
akimkaribisha MO kuzindua jarida hilo, pamoja na kumshukuru kwa
kudhamini uzinduzi huo pia alisema, IRIS Executive ni jarida pekee lenye
makazi yake nchini Tanzania kuweza kufika nchi zote za Afrika Mashariki
kwa idadi za nakala na taarifa zilizomo ndani zinazolenga uwekezaji na
biashara kwa watendaji ni matumaini yetu kwamba wasomaji watakuwa siku
zote wanajua nini kinachoendelea kwa manufaa yao, makampuni na sekta
mbalimbali zinazochangia katika kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na
taifa.
Aidha pamoja na kulipata jarida hilo la IRIS Executive katika nakala halisi pia hupatikana katika mtandao kwa anuani ya www.irisexecutive.com
Uzinduzi
huo ulihudhuria na maofisa watendaji wa ngazi mbalimbali kutoka
makampuni yanayojishughulisha na uwekezaji,biashara, habari na
utamaduni.
Mbunifu
wa Mavazi nchini anayefanya vizuri katika soko la kimaifa Sheria Ngowi
(kulia) akiwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko cha Sheria Ngowi Brand,
Deogracious Kessy wakati wa uzinduzi wa jarida la IRIS Executive.


No comments:
Post a Comment