Jumla ya raia wapatao 90 wa
jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Congo waliokuwa wakiishi nchini Tanzania kinyume na sheria wamekamatwa
katika operesheni maalumu ya kuwasaka na kuwarejesha makwao raia wa kigeni walioingia hapa nchini kinyume cha
sheria.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Kigoma balozi msaidizi, ubalozi mdogo wa Congo uliopo mkoani Kigoma Bw.Ricky Molema
alisema, raia hao 90, ambapo baadhi yao 16 wamekwisharudishwa makwao katika mkoa wa Kalemie, Uvira na ng`ambo ya Baraka,huku tayari wakiwa wameandaliwa mazingira ya kuishi huko nchini mwao.
Alisema hadi sasa kuna wahamiaji wapatao 10 watapanda meli gamba ili
kuwafikisha maeneo yenye asili yao ikiwa ni hatua ya kutekeleza agizo la Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete la kutaka kurejeshwa makwao wahamiaji haramu ambao imedaiwa kuwa ndio chanzo cha kuzagaa kwa silaha haramu na uharifu kwa raia wema.
Aidha kufuatia zoezi hilo raia wengine wa Congo,Rwanda na Burundi ambao wameshikiliwa katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma ambako shughuli ya mahojiano na utambuzi inafanyika,wataendelea kusubiri kurejeshwa makwao.
Kwa upande wa wahamiaji
hao walidai kuwa zoezi hilo wanaomba lifanyike kwa kuzingatia haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuonyesha vithibitisho vya uraia wao kutokana na baadhi ya taarifa zinazotolewa na wananchi za uwepo
wa raia wa kigeni zimekuwa zikigubikwa na wimbi la hila za kutaka kuwakomoa raia hao wa kigeni ambao miongoni mwao wapo wanaoishi kihalali wakiwa na vielelezo muhimu kama vitambulisho vya kupigia kura vya Tanzania,vyeti vya kuzaliwa na uanachama wa vyama vya siasa hapa nchini.
Walisema baadhi ya wananchi wanaitumia fursa hiyo
vibaya kwa kuwakandamiza raia wa kigeni
wenye uhalali wa kuishi hapa nchini ambao wengi wao ni wafanyabiashara hali inayoibua chuki binafsi na huku mianya ya vitendo vya rushwa ikiendelea kudhihiri kwa baadhi ya askari wasio na uzalendo kuwakamata na kuwaingiza kwenye kundi la
wahamiaji haramu pasipo hata kutoa vitambulisho vyao na wengine wamenyang`anywa nyaraka zao muhimu.
No comments:
Post a Comment