WATANZANIA
wameaswa kuishi maisha ya kupendana,kusaidiana na kuvumiliana na bila kufanya
hivyo Tanzania haitakuwa kisiwa cha amani.
Mbunge
wa jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Williamu Ngeleja alisema hayo wakati wa
ibada katika kanisa Moravian jimbo la Magharibi wakati akifanya harambee ya
kuchangia kwaya ya Upendo ya Sikonge.
Mbunge
huyo alichangisha kupitia harambee hiyo kiasi cha milioni 18 ambapo yeye
binafsi alitoa sh milioni 6,335,000,mbunge wa Sikonge Said Nkumba alitoa sh
milioni 2,mbunge wa jimbo la Igunga 500,000,mbunge viti maalumu Munde Tambwe sh
500,000 na mwenyekiti wa halmashauri Uyui sh 500,000 na waumini wengine
zikiwemo taasisi za serikali.
Ngeleja
alisema hivi sasa Tanzania tumefikia mahali kumekuwa na chokochoko kadhaa
ikiwemo watu wachache kutaka kutugawa kwa misingi ya dini,ukabila na ukanda na
kutaka watu hao wapuuzwe.
Alisema
dalili mbaya za nchi yetu kuingia kwenye mifarakano ziko wazi tunapaswa kukemea
hali hiyo kwa nguvu kubwa kwani imefikia mahali sasa watu wanakamatwa na madawa
ya kulevya na wengine wanamwagiwa tindikali.
“Sisi
kama wanakondoo wa bwana tunapaswa kukemea kwa nguvu zote na wachache hawa
wafikie mahali watambue sisi kama watanzania tuko imara hatuatkubali kuharibiwa
amani yetu kwa tamaa za wachache.” alisema.
Amesema
anaumia sana kusikia Tanzania ya leo imekuwa ni sehemu ya biashara na kuingiza
dawa za kulevya na kumwagiana tindikali kwa viongozi wa dini.
Mbunge
huyo alisema haya yote ymekuja kutokana na kutoishi kwa hofu ya bwana na
kutokubali kuishi na mwenyezi Mungu lakini tunapaswa kuombena.
Alisema
anapenda kushirikiana katika shughuli za kijamii ili kuleta maendeleo tarajiwa
na kwamba mali,utajiri na akiba vyote vinatoka kwa Mungu sote tutambue hilo.
“Ni
jambo la kufurahisha na kushirikiana na bwana kwa kuliimbia jinalake na ndiyo
maana leo tuko hapa tunazindua albamu ya “Kanisa la Mungu na kufikka kwake
Sikonge kanisani ni mpango wa Mungu” alisema.
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la Sikonge Said Nkumba awali aliwapongeza viongozi
wa kanisa Moravian kwani mafanikio yao ni kutokana na malezi na uongozi bora.
Alisema
Yesu anaondoa pazia la ubaguzi,dini na dini ukabila, ukabila undugu na undugu
tuachea hayo ni dhambi kwa mwenyezi Mungu.
Msomaji
wa risala ya kwaya ya upendo Aneth Masanja alisema kikundi kinahitaji kurekodi na vifaa vingine vinavyogharimu kiasi cha sh milioni
23.
No comments:
Post a Comment