KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika
Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16) anadaiwa kujeruhiwa
vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung'atwa ng'atwa usoni
na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo
anaonekana pichani ukurasa wa mbele.
Tukio
hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho,
limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine
wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa
kijana huyo.
Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa
Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo
limetokea miezi miwili iliyopita.
Akizungumza
na Majira katika mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya
kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie
soda.Aliliambia Majira kuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi wake
akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata mbwa
huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje.
DC
Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung'ata ulimi wa
mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga
kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya
ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza.
"Unaweza
kusema kuwa ni uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa
huyo aliendelea kula ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea
kumshangaa bosi wake kutokana na kitendo hicho kilichosababisha mbwa
huyo kufa,"Wakati akiendelea kumshangaa bosi wake ghafla alimrukia na
kumkamata kwa nguvu na kuanza kumng'ata kama mtu anayetafuna hindi la
kuchoma.
"Mshtakiwa huyo
alianza kumtafuna jicho moja na kufuatia jicho la pili na kisha kumeza
vipande vya macho huku akiendelea kumshika kwa nguvu," alisema DC
Mwamotto wakati wa mahojiano na Majira.
Baada ya kumaliza kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng'ata pua na kisha kumeza na vipande.
Baada ya kumaliza kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng'ata pua na kisha kumeza na vipande.
Alisema
kuwa wakati anaendelea na kitendo hicho majeruhi huyo alikuwa akipiga
kelele za kuomba msaada, lakini mshtakiwa huyo alianza kumng'ata tena
kipande cha mdomo wa chini na kisha kusababisha meno kubaki
nje."Kutokana na kelele hizo wananchi waliamua kusogea karibu, lakini
walikuta tayari, Susuluka amejeruhiwa vibaya usoni huku damu zikimtoka
kwa wingi," alisema.
Mwamotto
alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi walimvamia na kumpiga na
kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kibondo na majeruhi walimkimbiza
katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.
Majira
iliendelea na mahojiano hayo ambapo, mshtakiwa huyo alifikishwa katika
Mahakama ya Wilaya na kufunguliwa mashtaka ya kudhulu mwili."Hivi sasa
mshtakiwa yupo katika Gereza la Nyamisivi Kibondo, lakini cha
kusikitisha tena akiwa huko alimng'ata na kula vipande vya nyama vya
mguu mshtakiwa mwenzake," alisema.
Alisema
kuwa mshtakiwa mwenzake alimjeruhi vibaya na kupelekwa hospitalini hali
iliyosababisha mshtakiwa huyo kutengwa na washtakiwa wenzake."Mimi
nimelazimika kwenda hadi gerezani na kufanya mahojiano na mshtakiwa
huyu, kwani hili tukio linasikitisha sana lakini cha ajabu alitaka
kufahamu je ameshtakiwa kwa makosa gani ya kuua mbwa au kumng'ata mtu,"
alisema.
Alisema kuwa pia
amelazimika kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ambapo madaktari katika
hospitali hiyo walishindwa kumtibia."Nimeomba msaada kutoka Wizara ya
Afya ili mgonjwa huyu akatibiwe India na tayari maandalizi yameanza
kufanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Kibondo," alisema.
Mwamotto
alisema kuwa mgonjwa huyo hana pua, macho yamefumba, mdomo kwa
kujeruhiwa vibaya usoni hali ambayo anahitaji matibabu zaidi.Amewaomba
Watanzania kumsaidia kijana huyo ili aweze kwenda kutibiwa haraka nje
pamoja na kupata msaada mbalimbali kwa kuwasiliana na mganga mkuu wa
hospitali ya Kibondo ama kuwasiliana na Mhariri mtendaji wa gazeti la
Majira
:CHANZO MAJIRA.
:CHANZO MAJIRA.
No comments:
Post a Comment