Pages

KAPIPI TV

Wednesday, August 28, 2013

WANAFUNZI 140 SHULE MSINGI ISIKE WAKABIDHIWA RASIMU YA KATIBA.

Mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba mpya,Al-Shaymaa John akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Isike mkoani Tabora Mwalimu Charles Kalelanda.Picha na Hastin Liumba.
 Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba,Al-Shaymaa John akikabidhi raimu ya katiba mpya katika shule ya msing Isike
mkoani Tabora leo.Picha na Hastin Liumba.

Na Mwandishi wetu,Tabora
WANAFUNZI wa shule ya msingi Isike wamekabidhiwa rasimu ya katiba mpya
ili wajifunze kabla ya kuanza kwa somo la katiba mpya itakapokamilika.

Mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Al-Shaymaa John alikabidhi
rasimu hiyo ikiwa sehemu ya awamu pili ya kukusanya maoni kwenye
mabaraza ya katiba.

John ambaye ni mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoa wa Tanga,alisema
katika kazi hiyo anayofanya ametembelea baadhi ya shule katika mikoa
ya Pwani,Lindi,Shinyanga na Tabora.

Alisema mkoa wa Tabora ameshatembelea wilaya za Tabora
manispaa,Sikonge na Uyui na yupo katika mchakato wa kukusanya maoni
kwenye mabaraza ya katiba.

Alisema baada ya kumalizika kwa kazi hiyo watalazimika kurudi na
kwenda kuandaa rasimu ya katiba ya awamu ya pili.

Akikabidhi baadhi ya rasimu hizo kwa shule ya msingi Isike alisema
lengo la tume    ya mabadiliko ya katiba ni kutaka walimu na
wanafunzi waijue kabla ya somo la katiba yenyewe haijakamilika.

Katika hatua nyingine mjumbe huyo alisema amefarijika sana kuitembelea
shule ya msingi Isike kwani aliwahi kusoma kati ya miaka ya 1968-1969
akiwa darasa la kwanza na la pili.

“Natoa wito kwa waalimu na wanafunzi hasa wanafunzi kuisoma rasimu hii
ili waijue kabla ya katiba mpya haijatoka kwani itaanza kufundishwa
mashuleni.” alisema John.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule msingi Isike Charles Kalelanda
alimshukuru mjumbe huyo wa tume ya mabadiliko ya katiba kwa hatua yake
ya kuja shule aliyowahi kusoma.

Kalelanda alisema rasimu hiyo si kwa wanafunzi tu bali hata kwa
waalimu wenzake kwao itakuwa ni jambo jema na la faida kubwa kwao na
wataisoma na kuifundisha.

Mwalimu aliunga mkono hatua ya mjumbe kutembelea shule aliyosoma na
kusisitiza changamoto za kitaifa zilizopo zingaliwe kwa hicho la
huruma ili wanafunzi waweze kufaulu zaidi ya sasa.


No comments: