Pages

KAPIPI TV

Saturday, September 1, 2012

DC KUMCHAYA AKOMESHA MAJUNGU HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA

Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya akizungumza katika kikao Maalum cha baraza la Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Na Mwandishi maalum,Tabora
DIWANI na mkuu wa idara mkuu wa idara mmoja wamedaiwa kufadhili vurugu,majungu,fitna za chinichini,ili halmashauri ya manispaa Tabora isitawalike.Imefahamika.

Mkuu huyo wa idara,ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tume huru iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa,na diwani huyo wa kata moja iliyoko katikati ya mji,wamedaiwa kumwaga fedha na zawadi mbalimbali kwa watumishi na baadhi ya madiwani ili fitna zao ziendelee kwa maslahi yao binafsi.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao  huu kwa siku kadhaa  toka kuwepo kwa mipango ya kutaka kumuondoa mstahiki meya wa manispaa Tabora,Ghulamdewji Remtulah,kwa kura ya kutokuwa na imani
naye,kulitokana na mkuu huyo wa idara kutaka madaraka makubwa ndani ya manispaa hiyo.

Imedaiwa kuwa baada ya baraza maalumu la madiwani kufanyika,madiwani hao walimuomba kimaandishi mkuu wa mkoa kuunda tume huru ya uchunguzi ili kuchunguza ubadhirifu ndani ya manispaa hiyo ndipo mkuu huyo wa Idara na diwani huyo walipoingia msituni kuasi mpango wa kuundwa tume ama tume hiyo isifanikiwe kwenye uchunguzi wake.

"Sasa hivi diwani huyo na mkuu wa  Idara wameungana na wamekuwa wakipitapita huku na kule usiku wa manane, kujaribu kudhoofisha uchunguzi unaotaka kufanyika siku chache zijazo kwani yatabainika
mengi ya uozo." alisema mmoja wa madiwani.

Katika kikao maalumu cha baraza la Madiwani ,mwishoni mwa wiki hii,mwezi sepemba 28,mwaka huu,mkuu wa wilaya ya Tabora mjini,Suleiman Kumchaya,aliwaonya madiwani wachache ambao wamekuwa wakipitapita usiku kucha kutaka kuifanya manispaa isitawalike kwa maslahi yao.

Kumchaya alisema wapo wamdiwani ambao wamekuwa wakishirikiana na baaadhi ya wakuu wa idara kufanya hujuma,lakini serikali haitakubali hayo yafanyike.

"Nina taarifa kuwa wapo madiwani wanakesha kufanya vikao......ninatambua hilo lakini niseme tu serikali haitakubaliana na hayo kwani lengo letu ni maendeleo na siyo wachache kufadhili vurugu kwa maslahi yao." alisema Kumchaya.

Alisema madiwani hao ni kikundi kidogo tu na amekuwa akifuatilia kila kona kubaini kile ambacho wanafanya na aliwataka madiwani waliowengi kuendelea na juhudi zao za kuiletea maendeleo manispaa Tabora.

Mkuu huyo wa wilaya alisema serikali itaendelea kuchukua hatua ili kuweza kuondoa uozo uliopo ndani ya halmashauri na kamwe kuundwa kwa tume haimaanishi watakaosimamishwa watsfukuzwa kazi bali haki zao ziko palepale.

"Ninawasihi ndugu zangu tena ninawapenda sana na ndiyo maana wakato Rais Jakaya Kikwete, ananiteua kuja Tabora kama mkuu wa wilaya nilifurahi sana kwa sababu ninaipenda sana Tabora....naomba sana
achananeni hicho kikundi cha watu wachache wenye kuhujumu manispaa yetu." aliongeza.

Alisema sheria itafanya kazi mahali popote na anawaheshimu sana hivyo angependa kuona madiwani hao,watumishi na wakuu wa idara wanapata ushirikiano ili kuhakikisha kwa pamoja tunasimamia maendeleo.

Alisema tume iliyoundwa haitamuonea mtu yoyote na kwamba inatoka mbali na haitatoka miongoni mwetu.

"Kwa siku niliwahi kukaa na wakuu wa idara katika kikao kwa kweli nilishangazwa sana kuona wakuu wa idara wamegawanyika tena kila mmoja anusema ubaya wa mwezie kwa kuonyooshena vidole.......tusifuge
matatizo ndani ya manispaa jamani tauchane nayo tujenge halmashauri
yetu." alisema.

Hata hivyo aliwaonya baadhi ya wakuu wa iadara kuachana na lugha mbaya na kwamba wamauheshimu mkurugenzi Hadija Makuwani, ambaye ni mwajiri wao.

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya mansiopaa Tabora,Hadija Makuwani,aliuambia  huu kuwa ana taarifa za diwani huyo na mmoja wa wakuu wake wa iadara wanaofadihili vurugu ili manispaa yake
isitawalike.

“Nina taarifa zao sasa waache waendelee na hujuma muda ukifika nitachukua hatua nina imani madiwani wangu watamaliza tofauti zao,ila wakuu wangu wa idara nitamalizana nao na yataisha tu.” Alisema.

No comments: