Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 4, 2012

"NITAWAONDOENI KWA KUWADHALILISHA,KWA AIBU"-FATMA MWASSA "N i Watendaji wa halmashauri watakaobainika kuwa ni wezi wa fedha za Umma"

 Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa akizungumza katika kikao cha kikazi na wakuu wa wilaya saba za mkoa wa Tabora,kikao kinachofanyika kwa muda wa siku sita 
 Baadhi ya wadau katika kikao hicho ambapo pia walikuwapo wenyeviti wa halmashauri,Meya wa Manispaa ya Tabora,makatibu Tawala wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri pamoja na waandishi wa habari.
 Wadau katika kikao hicho wamkisikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Tabora wakati akitoa hotuba yake.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Urambo Bw.Adam Malunkwi na Mkuu wa wilaya ya Urambo Bi.Anna Magoa wakati wa kikao hicho.

Na Mwandishi wetu Tabora mjini.

Serikali mkoani Tabora imesema kuwa haitamvumilia mtendaji yeyote atakayebainika kuwa ni mwizi wa fedha za umma na kwamba atachukuliwa hatua za kisheria baada ya kuondolewa kwa nguvu katika wadhfa anaoutumikia.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa ametoa kauli hiyo kali wakati wa kikao cha kikazi na wakuu wa wilaya saba za mkoa wa Tabora ikiwa ni sehemu ya mafunzo elekezi kwa wakuu hao wa wilaya.

Bi.Fatma alibainisha katika kikao hicho kuwa kumekuwepo na ubadhirifu mkubwa wa  fedha katika halmashauri sita za  mkoa huo,vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watendaji katika halmashauri.

Alisema yamekwisha bainika madudu yaliyofanyika kwa halmashauri na hasa pale watendaji  wanapofanya vikao na kujilipa posho isivyo halali jambo ambalo limeendelea kuzitia hasara halmashauri hizo kwa muda mrefu.

Ingawa hakuweka wazi kuwa ni kiasi gani kilichoibiwa hadi sasa katika halmashauri hizo za wilaya lakini katika hotuba yake hiyo aliwataka watendaji wa halmashauri hizo kuacha mara moja vitendo hivyo vya wizi wa fedha za umma la sivyo hatua kali dhidi ya watakaobainika zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa nguvu katika nafasi zao za utumishi.

"Mwenye masikio na amesikia najua wizi umeufanya kwa muda mrefu,sasa kupitia kikao hiki nasema tena nitawaondoeni kwa kuwadhalilisha,kwa aibu kubwa na mtalala lockup kama wanavyolala wezi wengine"alisema mkuu huyo wa mkoa huku akionesha kuchoshwa na jambo hilo ambalo kwa mujibu wa maelezo yake amekuwa akilikemea mara kwa mara.

Kwa upande mwingine mkuu huyo amewataka wakuu wa wilaya kufanya kazi na wakurugenzi wa halmashauri kwa uwazi ili kuleta ufanisi katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Tabora.  

     

No comments: