Pages

KAPIPI TV

Sunday, July 22, 2012

Mh.EDWARD LOWASSA ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA WATANZANIA NA WAFIWA WA AJALI YA MELI MV.SKAGIT


SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA WATANZNIA NA WAFIWA WOTE WA AJALI YA SKAGIT

Ndugu zangu watanzania bara na wa Zanzibar, napenda kuzielezea hisia zangu kwa masikitiko makubwa juu ya ajali ya meli ya MV SKAGIT iliyotokea siku ya jumatano na kuwapoteza maisha ya watanzania wenzetu.

Kama ilivyo ajali haina kinga na ni janga la kiasili, hivyo naomba Watanzania wote tuwe wamoja na watulivu katika kipindi hiki kigumu kwetu kama taifa.

Huku juhudi za kuwaokoa wengine zikiendelea ni wajibu wetu sisi sote kuendelea kuwaombea majeruhi na manusura wote wapone haraka ili warudi kulitumikia taifa na pia tuendelea kuwapa pole wafiwa wote

Pia kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Monduli natuma salamu zangu za RAMBIRAMBI kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwa familia za wafiwa wote.

Pia naomba nitoe pongeza za dhati kwa Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete na serikali ya Chama cha Mapinduzi na kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)

Kwa pamoja wameguswa na tukio hili na kushiriki moja kwa moja katika kuwa pamoja na wanachi waliopatwa na mkasa huo wa ajali ikiwa ni pamoja na kutoa siku tatu za maombelezo kwa taifa.

Tuendelee kuwaombea kwa Mungu katika kipindi hiki kigumu kwetu na tena katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wenzetu Waisalmu.

Kwa pamoja niwape pole wote na kuwatakia mfungo mwema wote.

ASANTENI SANA WATANZANIA WOTE
Kutoka katika mitandao ya kijamii Group la TANURU LA  FIKRA

No comments: