Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 4, 2012

MAONESHO YA 36 YA KIMATAIFA SABASABA YANAVYOENDELEA JIJINI DAR-ES-SALAAM

Waziri mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) Sarungi Daniel (kulia) akimwelekeza mwananchi juu ya taratibu ya kujiunga cha IMF katika kozi mbalimbali leo jijini Dar es salaam wakati mwananchi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea.
Afisa Mafao wa Mfuko wa Akiba wa wafanyakazi serikalini (GEPF) Deogratius Urio (kulia) akisikiliza maswali mbalimbali  kutoka kwa Askari Polisi leo jijini Dar es salaam waliotaka kujua faida za kujiunga na Mfuko wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha  kwenye  maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere.
Afisa Manunuzi kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania(UTT) Hamis Kiimbi (kulia) akimwelekeza mwananchi juu ya taratibu ya kuwekeza katika mfuko huu jana jijini Dar es salaam wakati mwananchi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea.

No comments: