Pages

KAPIPI TV

Friday, July 20, 2012

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MJINI TABORA WANUNUA MITA 3000 ZA MAJI"Lengo ni kuboresha ufanisi wa kazi katika kuhudumia maji kwa wateja wao"

 Meneja biashara wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Tuwasa Bw.Benald Biswalo wakati akiangalia moja ya pampu mpya ya maji ambayo kwasasa inatumika kusukumia maji mjini Tabora.

Na Lucas Raphael,Tabora.

Maji - Tabora.

Mamlaka ya majisafi na majitaka mjini Tabora (TUWASA) imeleta mita  3000 za maji kwa ajili ya kuzifunga kwa wateja wa mamlaka hiyo mjini Tabora.

Meneja Biashara wa mamlaka hiyo Biswalo Benard, amesema kuwa mita hizo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni 36 na kwamba lengo lake ni kuhakikisha kuwa kila mteja analipa kiwango cha maji alichotumia hivyo kuondokana na mfumo wa kadilio la malipo ambao alisema hauna tija.

Alisema Mamlaka hiyo imelazimika kutumia mita hizo za plastiki kutokana na kuepa athari zinazoendelea za biashara ya vyuma chakavu inayoendelea nchini ambayo alisema imeipa hasara kubwa mamlaka hiyo kutokana na miundombinu yake ikiwemo mita kuibwa.

Akiongea katika ziara maalum ya kuitembelea Mamlaka hiyo, mkuu wa wilaya ya Tabora, Suleiman Kumchaya,  aliipongeza kutokana na jitihada kubwa inazoendelea kuzifanya  kwa lengo la kuboresha  utoaji wa huduma ya majisafi  na taka katika manispaa ya Tabora.

Hata hivyo aliitaka mamlaka hiyo ichukue hatua madhubuti za kulinda vyanzo vya maji kwa kutunga sheria ndogo ndogo za kulinda rasilimali hiyo muhimu kwa ajili ya uhai wa watu.

Hii ni ziara ya kwanza ya mkuu wa wilaya ya Tabora, kuifanya katika mamlaka ya majisafi na majitaka mjini Tabora (TUWASA)  toka alipoteuliwa rasmi kushika madaraka hayo miezi miwili iliyopita ambapo alitembelea  mabwawa ya Igombe, Kazima na kukagua shughuli za utandazaji wa mabomba ya maji katika mitaa mbali mbali ya mji wa Tabora yenye urefu wa kilomita 27.





No comments: