Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 25, 2012

AJALI - SIMBA MTOTO NA DAR EXPRESS YAGONGANA USO KWA USO"Habari zimeeleza kuwa licha ya kuwa ni ajali mbaya lakini hakuna aliyepoteza Maisha"

Abiria waliokuwa ndani ya Basi la Dar Express, wakitolewa kupitia dirishani baada ya ajali hiyo mbaya baina ya basi hilo na basi la Simba Mtoto, iliyotokea maeneo ya Mto Wami,wakati basi la Dar Express likitokea jijini Arusha kuelekea jijini Dar es Salaam na Simba Mtoto, likitokea Jijini Dar kuelekea jijini Tanga. Imeelezwa katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha zaidi ya mtu mmoja kubanwa katikati ya mabasi hayo baada ya kugongana uso kwa uso.Chanzo cha ajali hiyo hakikuweza kufahamika mara moja.
 Abiria walio ndani ya Simba Mtoto, wakihangaika kutoka ndani ya basi hilo.
 Abiria waliowahi kutoka ndani ya mabasi hayo na raia wema wakihangaika kuwasaidia abiria wenzao kwa kuwapitisha madirishani.
Mmoja kati ya abiria waliokuwamo katika mabasi hayo akiwa amejeruhiwa usoni baada ya ajali hiyo. 
Habari Picha kwa hisani ya  Mtaa kwa Mtaa Blog.

No comments: