Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 5, 2012

SERIKALI SINGIDA YAWAAGIZA VIONGOZI KUTOA ELIMU KWA JAMII KUHUSU UHARIBIFU WA ALAMA ZA BARABARANI

 Mkuu Mkoa Singida, Dk. Parseko Kone alifungua kikao cha 13 cha bodi ya barabara mkoa Singida
 Meneja wa TANROADS Mkoa Singida, Yustaki Kangole akifafanua hoja juu ya ujenzi wa moja ya barabara zinazohudumiwa na ofisi yake
 Kamati ya ulinzi na usalama, Ramadhani Isango (kushoto) na RPC Singida, Linus Sinzumwa (katikati), wakisikiliza kwa makini
 Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moshi Chang'a (Mbele kulia), DC wa Wilaya Iramba, Yahaya Nawanda(kushoto) na DC wa Wilaya Ikungi
 Sehemu ya Wajumbe wa bodi ya barabara mkoa Singida

Singida,
SERIKALI imeagiza viongozi, watendaji na wataalamu kutoa elimu ya kutosha katika maeneo ambayo barabara ya lami imejengwa, ili kuepuka uharibifu wa alama za barabarani, unaofanywa na baadhi ya Wananchi wasiokuwa waaaminifu, kwa kuzing’oa kwa makusudi.
Amesema barabara ni chachu ya maendeleo ya jamii katika kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla, hivyo ni lazima zitunzwe ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
“Wito wangu kwenu, tushirikiane kuwadhibiti watu hawa, mimi binafsi nilikwishaanza zoezi la kutoa elimu, Februari 2012 nilifanya mikutano katika vijiji vya Kititimo na Kinyamwenda…..Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Polisi, hii iwe ni sehemu ya kazi zenu,”alisisitiza Dk. Kone.
Baadhi ya wajumbe walilalamikia ung’oaji vyuma vilivyowekwa kwa ajili ya alama barabarani na kwenda kuuza kama vyuma chakavu, na kuomba jeshi la polisi kudhibiti hali hiyo.
Hata hivyo wajumbe wengine wametoa tahadhari ya biashara ya vyum, iliyoshamiri nchini, hali inayohatarisha usalama wa magari, ambayo hukatwa katwa vipande na kupakiwa kwenye Fusso kwa ajili ya kusafirishwa jijini Dar es Salaam, kuuzwa kama vyuma chakavu.
Na Elisante John 

No comments: