Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 5, 2012

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA MAFUNZO KWA WARATIBU WA SENSA MIKOA NA WILAYA

Meneja wa kitengo cha uchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Mwanaidi Mahiza akitoa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa karatasi za madodoso ya Sensa  ya watu na makazi 2012 kwa waratibu wa Sensa kutoka mikoa na wilaya zote nchini katika mafunzo ya awali yanayoendelea mjini Morogoro.
 
Waratibu wa  Sensa ya watu na Makazi 2012 kutoka katika mikoa na wilaya zote nchini wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Morogoro. Katika mkutano huo wa mafunzo mambo mbalimbali yanajadiliwa yakiwemo masuala ya  Bajeti, Ushiriki wa Viongozi katika Zozi la Sensa, Utunzaji  na ujazaji wa madodoso wakati wa Sensa, namna ya kuwapata makarani wa Sensa na vitendea kazi.
Viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu  Bara na ile ya Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,viongozi wa mkoa wa Morogoro na waratibu wa Sensa ya watu na makazi 2012 wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Alphayo Kidata (mstari wa kwanza katikati)mjini Morogoro.
Waratibu wa Sensa ya watu na makazi wakipitia moja ya dodoso litakalotumika wakati wa Sensa ya watu na makazi mwezi Agosti  mwaka huu na kujifunza namna sahihi  ya kuweka vivuli/ alama wakati wa kukusanya taarifa za kaya. 
 Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

No comments: