Pages

KAPIPI TV

Friday, June 1, 2012

MRADI WA MILENIA MBOLA WATOA MSAADA WA KOMPYUTA KWA JESHI LA POLISI

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Anthony Rutha akipokea msaada wa kompyuta kutoka kwa kiongozi na mratibu wa Mradi wa Milenia Mbola Dr.Gerson Nyandzi,kompyuta na printer yenye thamani ya zaidi ya shilingi mil.2.kwa ajili ya Kitengo cha Dawati la Jinsia kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Uyui.

 Baadhi ya maafisa wa Polisi wakiwa pamoja na waandishi wa habari Salma Abdul wa V.O.T Fm na Vivian Pyuza wa C.G Fm Radio Ofisini kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora wakati wa kukabidhi msaada huo wa kompyuta.
 Ofisini kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora wataalamu kutoka Mradi wa Milenia Mbola wakiongozwa na Kiongozi wa Mradi huo Dr.Gerson Nyandzi katika kukabidhi msaada huo wa kompyuta.
 Kiongozi na mratibu wa Mradi wa Vijiji vya Milenia Mbola Dr.Gerson Nyadzi akipeana mikono na maafisa wa Polisi,katikati ni kamanda wa Polisi wilaya ya Uyui SSP Zedekia Makunja.
 Kutoka kulia ni Dr.Gerson Nyadzi akiwa na mratibu wa Tehama wa MVP Bw.Kim Ayoub wakimsikiliza kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora.

Kiongozi na Mratibu wa Mradi wa Milenia Mbola Dr.Gerson Nyadzi akiwa na waandishi wa habari wa Tabora pamoja na wataalamu kutoka MVP.

No comments: