Pages

KAPIPI TV

Monday, June 4, 2012

CHADEMA YAVUNA WANACHAMA 52 KATA YA KAKOLA MANISPAA YA TABORA"VUA GAMBA VAA GWANDA"

 Mmoja kati ya aliyekuwa  kada wa CCM akichukua kadi ya kujiunga Chadema,huku akifuatiwa na wanachama wengine wapatao 51 katika kampeni ya VUA GAMBA VAA GWANDA 
 Mkutano wa Chadema
 Mmoja kati ya aliyekuwa kada wa CCM na pia ni kamanda wa Chipukizi wilaya ya Tabora Mjini wakati akionesha kadi yake baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chadema.
 Baadhi ya vijana wa CCM waliorudisha na kuchukua kadi za Chadema katika mkutano huo wa hadhara.

Na Hastin Liumba,Tabora

CHAMA cha demokrasia na maendeleo,(CHADEMA),kimendelea kuzoa wanachama
katika manispaa Tabora,safari hii kikizoa wanachama 52 toka kata mbili
za Ikomwa na Kakola.

Hatua hiyo inakuja kufuatia baraza la vijana la chama
hicho,(BAVICHA),kufanya ziara katika kata zote zilizopo ndani ya
manispaa, kwa lengo la kukiimarisha chama hicho kupitia kauli mbiu ya
sasa ya ”Vua gamba vaa gwanda”.

Awali akihutubia wananchi katika kata ya Kakola,diwani wa viti maalulu
Dora Ramadhan Chemchem,aliwaleza wananchi hususani wanawake wenzake
kuwa umasikini tulionao sasa ni msiba wa wetu sote na wale mabalozi wa
CCM wanaokuwa vinara wa kugawa kanga,kofia na vilemba kipindi cha
uchaguzi.

Chemchem ambaye diwani viti maalumu kupitia kata ya Kakola aliwaomba
wakazi wa kata za Ikomwa na Kakola kubadilika sasa kwa kuindosha CCM
ndani ya manispaa Tabora kwani hali zetu za maisha ni mbaya.

”Jamani inafikia mahali hata chai majumbani mwetu inakuwa kama kitu
cha anasa kutokana na ugumu wa maisha tulionao sasa.....tubadilike
sasa ni wakati wa kuamka ndugu zangu”.

Aidha diwani huyo CCM sasa ni choovu kwani wamebaki kusutana hovyo
hadharani wakishutumiana wizi na dhuluma wanazoendelea kuzifanya.

Alisema hata ajira zilizobaki za jeshi na polisi wanakwenda watoto wa
wakubwa na wa askari hao hivyo mnapaswa kuitafuta haki yenu ndani ya
CHADEMA na siyo chama kingine.

Akizungumzia hali ya miradi ya maendeleo kata ya Ikomwa,Chemchem
alisema barabara iliyopo ni njia za ng`ombe na hata visima vya maji
hata kile kimoja hakuna.

Aliwaomba wa wananchi kuliona hilo na kumuangusha diwani aliyepo kwani
wananchi kwenye huduma moja ya maji ameshindwa.

Diwani huyo aliongeza kuwa wnaachi wa kata ya Ikomwa wanapaswa
kujiuliza maji wanayochota kwenye dimbwi la maji watambue kuwa asubuhi
hai jioni wanachota wao,saa kumi na mbili pia wanakuja ng`ombe na
usiku wanakuja fisi hapo usalama uko wapi.

Alisema maisha ya wananchi hao wanayaweka hatarini kwa kuendelea
kuikumbatia CCM na sasa ifikie mahali waiptupe kama nguo chakavu.

Katika ziara hiyo CHADEMA ilipata wanachama 20 katika kata ya Ikomwa
na wanachama 32 waliingia chama hicho toka CCM katika kata ya Kakola.

No comments: