Pages

KAPIPI TV

Tuesday, May 15, 2012

SHULE ZASHINDWA KUSAJILIWA KWA KUKOSA VYOO VYA KUDUMU URAMBO

Na Robert Kakwesi,Urambo
 

ZAIDI ya Shule ishirini za msingi Wilayani Urambo zimeshindwa kupata usajili kutokana na kutokuwa na vyoo vya kudumu.

Afisa elimu wa Shule za msingi wilaya ya Urambo.Mwalimu Sisto Kigongo,amesema shule thelathini ziliombewa usajili lakini
 shule ishirini na nne hazikupata usajili kutokana na kutokuwa na Vyoo vya kuduma huku shule sita zikipata usajili.

Amesema wataalamu wamependekeza shule sita tu ndio zisajiliwe kutokana na kukidhi vigezo akiongeza miundombinu kama
 madarasa,nyumba za walimu na vyoo vya kudumu ni mojawapo ya vigezo muhimu kwa shule kusajiliwa.

Akizungumzia bbadhi ya shule kuwa na walimu wachache na nyingine kuwa na walimu wengi.Mwalimu Kigongo amesema pindi
 watakapopata pesa watawahamisha kutoka shule zenye walimu wengi kwenda zenye walimu wachache lakini kwa sasa hawana
 pesa kwa vile mwalimu mmoja akihamishwa inabidi alipwe sio chini ya shilingi Milioni Tatu.

No comments: