Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 16, 2012

SERENGETI YATANGAZA WENGINE WAWILI WALIOBORESHEWA MAISHA KATIKA WIKI YA TATU"Ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO"

Meneja wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo katikati akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Mkaguzi kutoka bodi ya taifa ya bahati nasibu, Bw. Abdallah Hemedi kulia akikagua jinsi droo hiyo inavyochezeshwa. Kushoto ni meneja wa bia ya Serengeti Bw Allan Chonjo na katikati ni mwakilishi kutoka PWC Bw.Tumainieli Malisa.

Ni katika droo ya tatu ya promosheni ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL.
Wiki mbili zilizopita zilikuwa za aina yake baada ya kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kuendelea kukonga nyoyo za wateja wake na watanzania kwa ujumla kwa kuwapa zawadi washindi wa promosheni inayoendelea inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya kizibo’ ambapo watanzania wengi wameshuhudia kampuni hiyo ikiwakabidhi washindi wa promosheni hiyo zawadi zao katika promosheni hii kubwa.
Amadeus Minja na Agness Msengi wakazi wa Dar es salaam, walijishindia jenereta (kangavuke) kubwa ambapo walikabidhiwa zawadi hizo mwisho mwa wiki iliyopita. Ibrahim Kimambo mkazi wa tabata jijini Dar es salaam alibahatika kujinyakulia pikipiki mpya na ya kisasa ambapo naye alikabidhiwa zawadi yake mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi unaovuma sana ujulikanao kama Dar LIVE pale Mbagala Zakhem.
Bw. Ibrahim ambaye hakuwa na kazi yoyote mpaka bahati iliyobebwa na promosheni hii ilipomdondokea  alikuwa na haya ya kusema, “kwa kweli nilipopata taarifa ya kushinda zawadi ya pikipiki sikuamini lakini sasa nimeamini na nawashukuru sana SBL kwa kuwa sasa naweza kujiajiri na kuendeleza maisha yangu na wale wanaonitegemea”. Kutoka jijini Mwanza Godfrey Shao ambaye alijinyakulia bajaj ya gurudumu tatu anaendelea kusubiri taratibu za usajili zikamilike ili aweze kukabidhiwa bajaj yake.
Asubuhi ya leo droo ya tatu katika promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini.
Droo hiyo ya tatu kama ilivyo kawaida katika droo zilizopita, ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers kuhakikisha washindi wote watapatikana kihalali.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni nchi nzima ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’ Na kuleta mabadiliko yakinifu kwa wateja wake.
Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa mawasiliano na mahusiano wa kampuni ya SBL Bi. Teddy Mapunda, amesema kwamba “mpaka sasa tumeshawapata washindi wawili wa jenereta ambao tayari tumewakabidhi zawadi zao, wengine ni washindi wa bajaj moja na wa pikipiki moja ambao nao wameshakabidhiwa zawadi zao”
“Tunawashauri wateja wetu na watanzania wote wenye sifa za kushiriki katika promosheni hii  ya aina yake waendelee kushiriki bila kukata tamaa na hatimaye nao waweze kushinda kwani promosheni yetu ni ya kweli na ya uhakika.” alisema Mapunda na kuongeza kuwa mpaka sasa tayari watu zaidi ya 2000 wamejishindia pesa taslimu na wakafanikiwa kupata pesa hizo kwa urahisi kabisa kupitia mtandao wa kutuma na kupokea pesa wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom MPESA ndani ya masaa ishirini na nne. Pia, washindi wamepatikana ambao wamejishindia zawadi za vinywaji vilivyopo katika promosheni hiyo.
Washindi wetu katika droo ya tatu ni Fadhili Manzi mkazi wa Mafinga mywaji wa bia ya Serengeti Premium Lager nambaye amejishindia bajaj na Raymond Denis mkazi wa Iringa ambaye  amejinyakulia jenereta kupitia bia ya Tusker Lager.


MAELEKEZO:
Nunua bia ya Serengeti lager, Tusker lager au Pilsner Lager fungua kisha angalia chini ya kizibo utapata namba zilizopo chini ya kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako, nakili namba zilizochanganyika na herufi  mfano AB55550, kisha tuma kwenda namba 15317 na unaweza kujishindia pesa taslimu kati ya shilingi 10,000, 50,000 au 100,000 au unaweza kujipatia bia ya bure kati ya bia zilizoainishwa katika promosheni hii . Fanya hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na magazeti.  Wanaoruhusiwa kushiriki promosheni hii ni walio  na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea.

No comments: