Pages

KAPIPI TV

Monday, May 28, 2012

SARAH PAUL AIBUKA MSHINDI REDDS MISS TABORA 2012


Washindi wa Redds Miss Tabora 2012.Katikati ni mshindi wa kwanza Sarah Paul,mshindi wa pili Glory Mongi na mshindi wa tatu Alice Emor katika mashindano yaliyofanyika ukumbi wa Chuo Cha Theofil Kisanji Tabora mjini.
Kutoka kushoto ni Redds Miss Tabora 2012,katikati ni Bw.Bushiri ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tabora na pembeni ni Mkurugenzi wa Club Royal Entertainment na mratibu wa mashindano hayo kwa mkoa wa Tabora Bw.Mgalula Fundikila.
Washiriki wa mashindano ya Redds Miss Tabora 2012 wakati wakiwa jukwaani katika mashindano hayo.
Mshindi wa kwanza wa Redds Miss Tabora 2012 akiwa ameketi mara baada ya kutangazwa mshindi katika mashindano hayo.

Na Juma Kapipi,Tabora mjini.
Hatimaye mrembo Sarah Paul ameibuka mshindi katika Mashindano ya Redds Miss Tabora 2012 na kujinyakulia kitita  cha shilingi laki tano fedha taslimu.

Pamoja na kuwepo kwa mchuano mkali kwa warembo hao kuonesha umahiri wao wakiwa jukwaani ikiwa ni pamoja na vipaji vyao mrembo Sarah sambamba na kupata kiasi hicho cha fedha pia amepata fursa ya kupata elimu ya masomo ya utalii kwa ngazi ya Diploma katika chuo cha Musoma Utalii Tabora mjini.

Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Glory Mongi ambaye amejinyakulia kiasi cha shilingi laki tatu,wakati wa tatu Alice Emor alipata shilingi laki mbili pamoja na udhamini wa elimu ya masomo ya utalii yenye thamani ya shilingi laki tatu katika chuo hicho cha Musoma Utalii Tabora.

Aidha washiriki wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Tanzania wamepata kiasi cha shilingi laki moja kila mmoja kama kifuta jasho.

No comments: