TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohd Shein
amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Dkt Shein kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (4) cha katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984, Rais amemteuwa Mdungi Makame Mdungi kuwa Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar.
Aidha
Dkt. Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 61 (2) cha
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 amemteuwa Khamis Jabir Makame kuwa
Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 16 Mei 2012,
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment