Mkurugenzi mkuu wa NHC na mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo Nehemia Kyando Mchechu, akitoa taarifa yake kwa wajumbe wa baraza hilo (hawapo pichani). Kulia ni naibu katibu mkuu wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Maria Bilia.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Maria Bilia, akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa NHC. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Kyango Mchechu na kulia ni Katibu baraza la wafanyakazi wa NHC Erasto Chilambo
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa NHC wakifuatilia kwa makini ajenda za baraza hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Maria Bilia (kulia) akiongozana na mkurugenzi mkuu wa NHC,Nehemia Kyando Mchechu, kuingia kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa NHC nchini.
Jengo la Lake Hill Hotel la mjini Singida mahali kikao cha baraza la wafanyakazi wa NHC kinafanyika. (Picha zote na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.
Shirika la nyumba la Taifa (NHC) limehimizwa kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba za kuuza na hasa za gharama nafuu, kama njia mojawapo ya kuisaidia serikali kupambana na vita dhidi ya umaskini.

Akifungua kikao cha baraza kuu la wafanyakazi wa NHC nchini Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Madeye (MB) amesema serikali inaamini kuwa mkiongeza kasi zaidi katika ujenzi wa nyumba, licha ya kuwa mtakuwa mmetekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala, pia mtaisaidia serikali katika juhudi zake za kuondoa umasikini nchini.

Amesema kuwa serikali kwa upande wake, inaendelea kujitahidi kuboresha sera ya nyumba na sheria mbalimbali ili kufanya sekta ya nyumba hapa nchini iweze kuchangia kikamilifu pato la taifa.

Katika hatua nyingine, Madeye amesema hivi sasa kuna ushindani mkubwa katika sekta ya nyumba hapa nchini, pamoja na ushindani huo, NHC haina budi kutambua kuwa wanalo jukumu la kuhakikisha wanawasaidia Watanzania wote,  kumiliki nyumba bora.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Kyando Mchechu, amesema wameweza kuboresha mambo mengi makubwa katika shirika hilo, ikiwemo uboreshaji wa ukusanyaji mapato kutoka shilingi bilioni 2.9 kwa kipindi cha mwaka jana,hadi shilingi bilioni 4.7 kwa sasa.